Monday, April 2, 2012

MAKUBARIANO


Makubariano ni kuweza kuelewa,ni kuwa na uelewa kukubari ama kukataa,sio kwa kichwa kama ikakatalika bali kwa namna yeyote ili mradi ikatambulika,mara nyingine kusiwe na maelewano  ni kwa sababu lugha ni tofauti,hapa labda tutaamua wenyewe kwani kama tuliweza kuishi katika makabira ya mbali na ikaja kueleweka basi hakika tunahitaji maelewano ikiwa mwanzo tulipatana na hatukuweza kufahamu kwamba inatupasa nini,maana kuna kujidai na kuwepo,hii kujidai ni namna ya kufanya kama vile ilivyo halisi,ikiwa na muigizo wa kuelekea katika lile lililotambulika na mmoja ama idadi yeyote kwamba linahitajika kueleweka.

Maelewano si o mpaka vita,maelewano hayana  hitaji la kutaka maana hapo tutaleta vita,tena ikiwa tunahitaji kuelewana ni lazima tujue tulikosana wapi?maana hata wapumbavu watajiona wenye nguvu sio kwa sababu hatuelewani ,au hatueleweki hata sisi pia kuelewa,bali kuna namna za kumfanya mpumbavu akaelekea na upumbavu wake,kwa vingine vile vya kuonekana na kufanyika vinaweza kuigwa,hapa tuangalie tusije kuiga upumbavu wakati tunataka maelewano,maana ni lazima kuwa karibu.

Ukaribu ndiyo unaoleta maelewano,hasa kama tutawasiliana kwa simu,na aina yeyote ikaitwe mawasiliano,hata kwa yanayoendana huwa yanaelewana,ikiwa tu imetakiwa iwe hivyo.katika kipindi cha kuubiri majibu ndiyo pale maamuzi yaliyofikirika hutoka,hapa inaweza kutoka vita ikiwa fikra zitabaki pale pale,tunaweza kuendelea kwa kusema mabaya ni mengi yaliyofanyika,sio kwamba tukataka maelewano kwani na yenyewe yanaweza kuja na kuwa mabaya,labda tukae mbali tuone ni namna gani tunaelewana.
Ikiwa siku na jua navyo vinaenda tofauti  havitaki kukutana si ya kwamba havielewani,fikiri ya kuwa usiku ungekuwa upi?maana jua lingewaka tu,hapa isiwe kwa mateso basi na tufanye vimeelewana hivyo jua siku moja na mwezi siku moja,bila uangalifu hapa tungetafuta namna ya kuelewana maana kwa wengine waliozoea usiku watataka mwezi uwe wao ,hawa wa jua itakuwa vita kali na wakulima,maana hata na mvua inakatishwa tamaa kwa vile tu..imekuwa too much.

Kipindi cha zamani sio kama cha sasa,vijana wa zamani ndiyo wazee wa sasa,yaani hata vitu vya zamani ni vya zamani tu,Yule akaichukulie ile mpya inamaana ndiyo kaiona hata haina haja ya kuuliza,ni sawa unamuuliza baba leo tutakula nini na wakati unaona mama yupo jikoni,tena huko nako kukiwa hamna maelewano maana ile sukari ya jirani ndiyo imesaidia kwa ule unga robo uliobaki juzi,maana na jana tulitegemea tutapata jioni kwa bahati watoto wakalala,mambo mengine yanahitaji muda maana hatutaweza kufikiri haraka namna hiyo,yaani kwa muda huu sio kufikiri tu ukijua ndiyo umeweza zaidi ya kuona kama unaweza.maana mawazo hayafikiriki mpaka huleta vurugu hata ya kujichukia mwenyewe.

Tunapoelewana tunamaana ya kuelewa kwa kila mmoja sasa Yule mmoja na wake mwingine isije na kuelewa tofauti,ikaeleweka kwa maana,tusiombe kesho ije ikiwa tuvuke vita ya leo,kama mtu kashiba basi chakula kifunikwe au njaa itafutwe,tena si kwa Yule tu muandaliwa maana wanaotaka kuelewa ni wengi tatizo ni kwamba kila mtu anaelewa lake,ni vigumu kumuelewesha Yule anayetaka kuelewa vyake,tutaleta vita tena isiyo kuwa na nafasi ya kupigana ikiwa wapiganaji ni wengi mno,ukiona kuna kunyamaza kwa kuinama chini ujue kuna misemo hapo,kope zikamfanye mtu afiche kile alichokiona mara ya kwanza kwa kujifanya kutokujua,hivyo baadaye ikawa ni mtafaruku,yaani maelewano kukosekana

By: Benson G.
Tel: +255714 33 66 57.
Email:bensonsmakaya@gmail.com



No comments:

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...