Friday, August 31, 2012

NATUMAINI


Ningetaka kulia ningejifungia maana ingekuwa haina maana kuonyesha machozi hadharani,kwa kila mtu akiuliza unalia nini maana wataniona tena wao wakiwa na matumaini katika yale yanayowaumiza juu yangu,ikiwa katika kuanza kutumaini ni kutaka kupumzika katika sehemu na mahala salama nimeshafahamu majibu ya maswali mtakayouliza na hakuna jibu zaidi ya mtu akakuuliza ikiwa ndiyo nlitakiwa kujibu hivyo nikiwa namaana ya ninachotumainia ndicho,pengine katika matokeo ikawa sio matumaini yako,kwa upande wa kulia ama kushoto zote ni njia maana upande wa kuingilia si mmoja pia

Leo nikisema mimi ntakusemea pia wacha ninene pengine yataenea,ni tumaini langu kuwa baba bora kwa mwanangu,natumaini kilio changu umeniskia,hakuna lazima isiyo kuwa na kutaka,pengine ikiwa umetumainia jambo fulani,na kwa jinsi muda unavyozidi kwenda tumaini hutumika kwa namna tofauti na mwisho wa siku kubaki na hakuna kitu au ukakata tumai kabisa,yenyewe huja na namna yavile ulivyoyatumainia,pengine yalikuwa ni matumaini ya kijinga basi na utajaa ujinga zaidi yake.

Pole leo unalia,pole sana kwa ujinga na matokeo yaliyokukutia,maana katika hali ya kutazama unaweza usieleweke kama pengine ni kilevi cha mwili ama nafsi,maana kupoteza kwa kujua mwanzo na kutokujua kama ulichokuwa unajua ni sahihi hapo utalamba galasha,maana wengi huwa wanakuwa na akili zenye ufahamu wa wao,kila mmoja akiwa na wake lakini wako katika kufikiri ndiyo matumaini yako katika kile unachokiwaza,lolote linalotokea linapimwa na nguvu ya matumini yako hivyo kuwa Kamili.

ELEWA 2

  Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye na kukataa kuelekea hata kwa ku...