Friday, August 10, 2012

TEGEMEO.


Yote ni ya Mungu haina haja ya kumwachia mengine,eti haya ya mungu ya shetani yako wapi?tegemeo lako likidondoka angalia kwa kushikiria,siku hizi wanauza watu,yaani uwe mtoto,mkubwa,bila kujali jinsia,ukitegemea sana ya mbele unaweza kufa maskini,maana haukufanya zaidi ya kutegemea,hakuna mjinga anayejihukumu kwa zuri lake,maana makosa anayaficha…makosa ndiyo mafunzo,unapomwambia mtu unategemea nini namatumai ya kuwa na wewe ulikuwa unategemeo lako,maana kama mko zaidi ya mmmoja mtatuletea mategemeo yenu.

 Mazuri ni mengi ndiyo maana kila mtu akawa ya kwake,bila hivyo tungemiliki nafsi moja,na ikiwa ni hivyo basi jaribu kutegemea kitu,maana hata ya kukumbusha tu.pengine imekuwa tofauti sawa na pale ukaambiwa mjini kuna magorofa na kufika mjini kuona nyumba zimepandana,ukiwa na mategemeo ya kiasi fulani huleta faida ya kile ulichokitegemea,maana matokeo yakiwa tofauti na mategemeo hapo lazima kuna mwingiliano,ikiwa mtu hajajitambua au kifaa hakijakaa mahala pake.

Pengine iangaliwe usije kufanya yale yaliyo ya watu,maana kwa kushindwa kutegemea au kutegemea tofauti maana ukisema nzuri bado itapasa kuifahamu na mbaya iko wapi,ili inapokuja labda ufurahie yatakayo kuwepo kwani hakuna namna ya kubadilisha zaidi ya vilivyobadilishwa,maana mategemeo ni namna ya vile mtu alivyofikiria na kuona ile itamfaa ya kuwa ilitokea baada ya yeye alipofanya.

UPENDO..


Kuna baadhi ya sifa ya ajabu katika watu wamiliki wa baadhi walivonavyo. Kama kitu ni cha milele, na ni tumaini  watu kuimiliki kwa wingi. Wakati mwingine matumaini yanaonekana kufa chini ya shina, ikiwa haikutumainiwa kwa vile iwe ya milele,ikapendeze tena bila kelele,bali ni milele inavyoupendezesha moyo upya katika nafasi ndogo uliyoiruhusu.moyo ni hazina ya furaha katika maisha yako kwani maamuzi yanayotokana na wewe ndiyo wewe mwenyewe unavyotafsilika katika pendo.

Na halafu pia  katika kutumaini ili kuishi kuna  Kifo, maumivu, na taabu za maisha hivi vitu kuvuruga upendo, ukiwa hauna namna , zisizogusika nje au hata ilivyo ndani ya mtu binafsi ni hatua kama ya milima, na ni mwanzo na mwisho wa uhai wetu.Upendo unaipa dunia kivutio chake. Ni upendo peke yake wa kupendezesha na kuleta furaha, na kwamba humfanya mwanadamu kutoka kuwa mahali pa ukiwa ikiwa amekubari kupendeza na furaha. Hii inatufanya iwe ni milele kujenga maono mapya na ndoto njema, milele kutoa  mawazo mapya ya  mwongozo

kuna namna fulani inaonekana inachanganya sana na makosa ya kudhani upendo ni bidhaa ya mwili tu na damu. Hata mchakato mrefu ndani yetu inatuambia upendo huja juu ya mbawa zinazotoka kwa Mungu.hivyo katika swala la kuamini ni kazi ya kila mmoja maana hakuna anayempendea mwenzake,kila mtu na moyo wake ikiwa ameyatumainia maisha yake yawe katika namna ipi,itakayokupendezesha mwenyewe.

KATIKA UKUAJI..

Muda mwengine inapasa tu kupumzika,maana ukiwa umefikiria sana kuona ni wengi wasioelewa na wakihitaji kueleweshwa,ni maisha tu ambayo kila mtu anaweza kujichagulia,maana na maisha yenyewe ni yanasema kinamna yake,napenda sana kuona maisha yanavyonipelekesha,maana nisingepelekwa hata kwa wengine nisingejua kama walipelekeshwa,maana jua na ulimwengu ndio vinasema yote,pengine watoto wa sasa wanang’aa sana,sijui ni haya mafuta ama ni maisha na zake namna,maana majina mapya yatatufikia baada  ya kuchoka,’kanunue unga kwa baba ndevu’.wewe huyo,ufikiri muda wa mahali ulipo.

Hakuna anayekulazimisha kuishi maisha mazuri,vyema kila mtu atumie namna yake maana katika kulingana tutafanya kuleta mshindi,michango na mawazo ni haki ya mtu.hivyo huwa kiheshima na kujenga uhusiano bora pale tu kunapohitajika maelewano,hapo ukiwa binadamu kamili.dunia iko sawa katika mihimili yake,ila  tatizo ni hizi barabara za juu,endapo za chini ulishindwa kutokana na kuchanganyana,kuchanganyana kwa mihimili ya kibinaadamu,kila mwanadamu ana muhimili wake,yeye na maisha yake,hata iwapo mke na mume.

Machache naimani ndiyo humfanya mtu kuelewa alichokusudia,maana hilo ikiwa ni elekezi tu,si njia. Nafsi inainuka kuona mabovu yamelindima,yakitakiwa kuwindwa kwa uchache wa siraha tulio nao hakuna jema litakalo fanyika,hakuna wema watakao fikirika ikiwa imeonekana mapema kuwa haina maana,haina maana ya kupigana wakati kila mtu ana lake,kila mtu ana yake ikiwa yameonekana tayari,

NANE NANE


Sitashangaa kusikia moja moja,maana pengine imekuwa ni kama matokeo tu,tunapoonyeshwa hatuoni kwa kusema ona,maana na macho na yenyewe lazima yaambiwe ona,ikiwa kila sauti yanasikia maana tumeona vitu vya ajabu sana katika mikusanyiko yenu,mikutano ikiwa nane inaashiria kuendelea kufika kumi,tujue ya saba imetoka wapi basi.wananchi na nchi yao hawawezi kuwa wapumbavu kwa kushindwa kuelewa wanachoonyeshwa,hapa wanahitaji kuelekeza ikiwezekana kupewa semina,sijui tunaishije bila semina maana ndiyo yamekuwa maisha yetu,sijui unajifunza nini humo,sijui ndo hivi vya semina ama ni katika kufanya biashara.

Siku ikiwa ni ya nane ni kwa sababu ya saba jumapili,ndiyo maana ukasikia sabasaba,hawa watu wanapenda sana kupumzika ikiwa ni siku yao ya kuonyesha,si wanauza..!wewe ndugu yangu umelima lini jana tunasikia unalia njaa?au nini nisaidie ndugu yangu maana kila kitu siku hizi ni maonyesho ya sabasaba,wapeni watu uzalendo wa kuifikiria siku kuku,pengine mtu akiwaza shari kuzidi heri,sikunyingine zinakuja maana mpaka kumi kumi.ikiwa huduma zitaonekana kuwa duni.

Muda unatoka tofauti ya vile tulivyofundishwa,maana na wenyewe wanahitaji kufundishwa,kwa hilo ukiamua kusema kilimo kinaanza sio kama uzamini wa simba na yanga,hapa ni zaidi ya ‘madaruga’ na ‘mabarugaja’,ni zaidi ya kombati siku yake ya kumi inapofikia,maana hapa tutasema dunia imejaa mengi kwa bila kufikiri yale yamoyoni umeyaweka sana akilini,inaleta matatizo kubadili maana kwa kuonekana ikiwa kama ushahidi,angalia namna ya maisha uliyochagua kabla siku ya saba haijaisha maana hii ya nane utaingia shambani.

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...