Friday, August 10, 2012

KATIKA UKUAJI..

Muda mwengine inapasa tu kupumzika,maana ukiwa umefikiria sana kuona ni wengi wasioelewa na wakihitaji kueleweshwa,ni maisha tu ambayo kila mtu anaweza kujichagulia,maana na maisha yenyewe ni yanasema kinamna yake,napenda sana kuona maisha yanavyonipelekesha,maana nisingepelekwa hata kwa wengine nisingejua kama walipelekeshwa,maana jua na ulimwengu ndio vinasema yote,pengine watoto wa sasa wanang’aa sana,sijui ni haya mafuta ama ni maisha na zake namna,maana majina mapya yatatufikia baada  ya kuchoka,’kanunue unga kwa baba ndevu’.wewe huyo,ufikiri muda wa mahali ulipo.

Hakuna anayekulazimisha kuishi maisha mazuri,vyema kila mtu atumie namna yake maana katika kulingana tutafanya kuleta mshindi,michango na mawazo ni haki ya mtu.hivyo huwa kiheshima na kujenga uhusiano bora pale tu kunapohitajika maelewano,hapo ukiwa binadamu kamili.dunia iko sawa katika mihimili yake,ila  tatizo ni hizi barabara za juu,endapo za chini ulishindwa kutokana na kuchanganyana,kuchanganyana kwa mihimili ya kibinaadamu,kila mwanadamu ana muhimili wake,yeye na maisha yake,hata iwapo mke na mume.

Machache naimani ndiyo humfanya mtu kuelewa alichokusudia,maana hilo ikiwa ni elekezi tu,si njia. Nafsi inainuka kuona mabovu yamelindima,yakitakiwa kuwindwa kwa uchache wa siraha tulio nao hakuna jema litakalo fanyika,hakuna wema watakao fikirika ikiwa imeonekana mapema kuwa haina maana,haina maana ya kupigana wakati kila mtu ana lake,kila mtu ana yake ikiwa yameonekana tayari,

No comments:

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...