Ni kawaida kwa wanaosema bila ya kusikia maana wao
wanajua,pengine ikiwa hata jambo bado kuisha ikasikika na kusemekana
kuwezekana.maisha yamekuwa dawa maaana watu wanaumwa bila kujua wanaumwa
nini,haiwezekani kwa mwanadamu wa kawaida kujipa ugonjwa na kushindwa
kujitibu,maana kama ni mawazo unawaza nini kisichowazuka?wachache waliwaza
wakatengeneza magari,ikaja kwa wagunduzi kukatazwa ya kuwa watajawa na
‘stress’,hapo ikiwa inakupasa kuogopa stress,tegemea stress zaidi maana ili iwe
kama kawa kuna namna yake ya kujua,hapo huwa imetendeka kwa mara ya
kwanza.yaani mapema.
Kama kawa Baraka za kwangu mchache nimezipata,yatafanyika
yale yaliyokusudika ikiwa ni mema mbele ya macho ya Yule aliyetuumba,na tena
Baraka zenyewe zinapokuja hapo utaskia kama kawa ‘alikuja’,ikiwa mtu amekuwa
zaidi ya vile vyema ilivyo,muda mwingine lazima tukubari mateso ili kuja kula
raha baadaye,na Yule atakayekuja kudai hizo raha baadaye ni lazima aulizwe tabu
amekula kipindi gani,maana kwa wengine taabu ni kama kawa,ikiwa kwa mgeni ana
haki ya kushangaa.
Mjini joto limewaka kama kawa,na hii ikiendelea lazima
kutafuta zaidi dawa,magonjwa mengine si kwamba yameshindikana bali wagunduzi
bado hawajaumwa ugonjwa huo,na pengine ikiwa wameumwa basi waligundua vingine
hao..maana siku hizi vikombe watu wanakunywa kama kawa si wakijiamini kwa namna
wanavyotembea,ukisahau kujikwaa utaanguka kabisa.maisha ni dawa yahitaji kunywa kujiponya.