Monday, August 27, 2012

KAMA KAWA..


Ni kawaida kwa wanaosema bila ya kusikia maana wao wanajua,pengine ikiwa hata jambo bado kuisha ikasikika na kusemekana kuwezekana.maisha yamekuwa dawa maaana watu wanaumwa bila kujua wanaumwa nini,haiwezekani kwa mwanadamu wa kawaida kujipa ugonjwa na kushindwa kujitibu,maana kama ni mawazo unawaza nini kisichowazuka?wachache waliwaza wakatengeneza magari,ikaja kwa wagunduzi kukatazwa ya kuwa watajawa na ‘stress’,hapo ikiwa inakupasa kuogopa stress,tegemea stress zaidi maana ili iwe kama kawa kuna namna yake ya kujua,hapo huwa imetendeka kwa mara ya kwanza.yaani mapema.

Kama kawa Baraka za kwangu mchache nimezipata,yatafanyika yale yaliyokusudika ikiwa ni mema mbele ya macho ya Yule aliyetuumba,na tena Baraka zenyewe zinapokuja hapo utaskia kama kawa ‘alikuja’,ikiwa mtu amekuwa zaidi ya vile vyema ilivyo,muda mwingine lazima tukubari mateso ili kuja kula raha baadaye,na Yule atakayekuja kudai hizo raha baadaye ni lazima aulizwe tabu amekula kipindi gani,maana kwa wengine taabu ni kama kawa,ikiwa kwa mgeni ana haki ya kushangaa.

Mjini joto limewaka kama kawa,na hii ikiendelea lazima kutafuta zaidi dawa,magonjwa mengine si kwamba yameshindikana bali wagunduzi bado hawajaumwa ugonjwa huo,na pengine ikiwa wameumwa basi waligundua vingine hao..maana siku hizi vikombe watu wanakunywa kama kawa si wakijiamini kwa namna wanavyotembea,ukisahau kujikwaa utaanguka kabisa.maisha ni dawa yahitaji kunywa kujiponya.

No comments:

ELEWA 2

  Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye na kukataa kuelekea hata kwa ku...