Thursday, August 30, 2012

MAZINGIRA..


Hili halitahusisha uoto wala namna ya kustiri kupumua ya maana hali kuwa shwari,pengine ikiwa hakuna vita ama ipo ila wanaopigana ni panzi maana wao kufurahi,kuna namna za kutokuruhusu zinazofanya mazingira kuwa mabovu,hii ikiwa wachache wamekalia mazingira ambayo japo watoto wangeweza kucheza,kwa nini tuseme watoto?hapo ndiyo tutagundua na michezo mipya ya kikubwa,maana watoto hucheza na wakubwa kufanya kulingana na mazingira.

Tunapotupa takataka jararani tunayaweka mazingira yapate kueleweka,maana  mahala pataeleweka palivyo,hiyo ikiwa haina wa kusingiziwa kwani aliyetupa ataoneka,pengine wengine wasiwe na uwezo wa kuona,lakini ya kibadamu hapaswi kuachiwa Mungu maana yeye ameyaweza yake.muda unavyosogea wale walio wahi wataonekana kuchelewa kutokana na mazingira yenyewe kuwa machafu,tena hii imezoeleka wote yapaswa kuitwa vichaa kwani hata wanaojifanya kuelewa wameelewa mazingira tofauti.kila mtu ana mazingira yake.

Namna ya kufanikiwa katika maisha haijawa katika kufanikiwa vile ilivyo,maana katika mazingira mengine haipaswi hata kuongozwa,na endapo kutakuwa na kiongozi ni lazima wachaguliwe wale wachafu wanaolipenda jalala kwanza,maana katika mazingira ya uongozi huo kutokufahamika vyema,yaani ikiwa hayaeleweki,kipindi hichi tunatakiwa vijana kujitoa ili kusafisha jalala hilo,maana bila ya harufu ya mauti kutoka wachache wataendelea kutupa taka humo ikiwa wamekalia mazingira kwa kusema ni yao..tukichunguza jalala hili vizuri atajulikana ni yupi anayeongoza kwa utupaji taka bora…huyo anaweza kuwa mchafu zaidi.zaidi ni kumtafutia mahala pa kumtupia alimradi asizidi kuzoeana na uchafu uliopo katika mazingira yake.

No comments:

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...