Saturday, August 4, 2012

KIALIMU ZAIDI...

Mwalimu kazi yake ni kufundisha,kama ilivyo kwa daktari kutibu,kwa meneja kutawala,ikawa na kwa muhasibu kuhesabu na vyovyote vingene inavyokuwa alimradi ni kazi ya mtu ameichagua,pengine kazi zote ni sawa kutokana na mahitaji ya mtu mwenyewe,imekuwa ni kwa kasi kubwa wale wasomi kutaka kazi tena zenye mishahara minono,hiyo ikiwa wametoka shuleni,wao wakidai wamepoteza muda mwingi wakiutumia kusoma sio kama vile wale waliobaki wakiamua kutafuta maisha yao katika namna wanavyoweza.na wao wanafanikiwa zaidi,hivyo ikawa isilete lawama kwa kuwa kama ni shule mtu umeamua kwenda mwenyewe,tena kama ni chanda kilikuwa kikicheza tu ni lazima tutafute namna ya walivyokuwa wanamchezesha,maana wengine wamejifunza vizuri ru.

Pengine leo hii utaambiwa sio haki yako,pengine ni wito,mwalimu anayeamua kufundisha kuanzia saa moja asubui hadi jioni huyo ametimiza wito wake,kwa maana ametaka watu kuelewa zaidi ya kile anachoridhika nacho,baba wa taifa alipata kuridhika na mali alizonazo na kama angegoma kufundisha watanzania mpaka sasa tungekuwa tunatawaliwa na mtindo tofauti sana,pengine hata tusingepata nafasi ya kugoma,tusifananishe maisha yetu ya kuwa hatuna uwezo wa kupigiwa simu saa nane za usiku kana kwamba kuna mwanafunzi amezidiwa kwa kuwa kesho na mtihani,kazi ni kufundisha,swala la kuelewa hilo hatuwezi kulazimishana..

Pengine ndugu zetu tuangalie na usalama wa nchi yetu,hata kama tunadai haki zetu.haya mengine machache tu na ikiwa umeona umeshindwa kuishi wewe,hata watoto wako wataishi tu,labda ikiwa haina maana ya kujipanga tena maana umeshachelewa,wengine tuendelee kukaza buti maana hili ni janga letu sote,kama tutagoma kula chakula tulichopika wenyewe hapa yapasa kusafirisha njaa, maana tusipoileta katika muda hata wa nyongeza,hapo tutaeleweka kama wanafunzi maana swala ni kuishi.

MAISHA YA KUTUMIKA..

Katika kutumika ni lazima kusafiri na kujua katika nafsi umeweza kufikia malengo fulani,umekuwa katika akili na yote kufanyika ikiwa kila mmoja amechukua nafasi yake,kufuta yale ya zamani pengine yanaweza kuwa mabovu,katika kufanya maisha yawe katika namna ya kutumika ni kuendelea na maisha yako katika malengo ikiwa ni maono na dhumuni ikiwa vyote sio kitu kimoja,na hapo tukafungue milango yetu ya kuelewa ili uweze kuelewa namna ya kuishi,tofauti ya vile unavyotamani.

kila maisha ya mwanadamu yana maana yake ikiwa sababu imeanza kwanza,hivyo mwanadamu anapaswa kufanya na kuingia katika mawazo ambayo yanaweza kumjenga ili yeye mwenyewe aweze kuelewa sababu yake,tunaweza kuishi tofauti na kusema hiyo ni sababu moja wapo ya kuishi lakini sio ile moja ambayo kila mtu anayo ya kwake,pengine haikupaswa kuishi hivyo unavyoishi,ama ilikuwa ni chini sana na kutokana na juhudi zako umefika hapo,na hiyo ni kwa sababu ilisemwa lazima kufanya ili kusaidikika,pengine mengine yakiwa ya ziada na msaada basi tunastahiri kushukuru kwa yote.

Bila kukubali katika maisha ya kutumika hapo hatutatumika,hapo hatutajielewa vyema vile tulivyo kwa maana ya kutokujua uwezo wa kweli tulionao katika sababu ya kuishi humu duniani,pengine inatulazimu kujua yapasa muda mwingine kupata vile vya pembeni na hiyo ikiwa kila mtu ana asili yake ya kupata kile kilicho cha pekee kwake,pale tunapotumika tuangalie muda ya kuwa kuna kuharibika baada ya kukaa muda mrefu,na kama tutaharibika na kuendelea kutumika hapo tutakuwa tunajizika wenyewe ya maana kama wafu.tuzitumikie nafasi zetu vile tunataka maisha yetu kuwa.

ELEWA 2

  Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye na kukataa kuelekea hata kwa ku...