Saturday, August 4, 2012

MAISHA YA KUTUMIKA..

Katika kutumika ni lazima kusafiri na kujua katika nafsi umeweza kufikia malengo fulani,umekuwa katika akili na yote kufanyika ikiwa kila mmoja amechukua nafasi yake,kufuta yale ya zamani pengine yanaweza kuwa mabovu,katika kufanya maisha yawe katika namna ya kutumika ni kuendelea na maisha yako katika malengo ikiwa ni maono na dhumuni ikiwa vyote sio kitu kimoja,na hapo tukafungue milango yetu ya kuelewa ili uweze kuelewa namna ya kuishi,tofauti ya vile unavyotamani.

kila maisha ya mwanadamu yana maana yake ikiwa sababu imeanza kwanza,hivyo mwanadamu anapaswa kufanya na kuingia katika mawazo ambayo yanaweza kumjenga ili yeye mwenyewe aweze kuelewa sababu yake,tunaweza kuishi tofauti na kusema hiyo ni sababu moja wapo ya kuishi lakini sio ile moja ambayo kila mtu anayo ya kwake,pengine haikupaswa kuishi hivyo unavyoishi,ama ilikuwa ni chini sana na kutokana na juhudi zako umefika hapo,na hiyo ni kwa sababu ilisemwa lazima kufanya ili kusaidikika,pengine mengine yakiwa ya ziada na msaada basi tunastahiri kushukuru kwa yote.

Bila kukubali katika maisha ya kutumika hapo hatutatumika,hapo hatutajielewa vyema vile tulivyo kwa maana ya kutokujua uwezo wa kweli tulionao katika sababu ya kuishi humu duniani,pengine inatulazimu kujua yapasa muda mwingine kupata vile vya pembeni na hiyo ikiwa kila mtu ana asili yake ya kupata kile kilicho cha pekee kwake,pale tunapotumika tuangalie muda ya kuwa kuna kuharibika baada ya kukaa muda mrefu,na kama tutaharibika na kuendelea kutumika hapo tutakuwa tunajizika wenyewe ya maana kama wafu.tuzitumikie nafasi zetu vile tunataka maisha yetu kuwa.

No comments:

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...