Mwalimu kazi yake ni kufundisha,kama ilivyo kwa daktari
kutibu,kwa meneja kutawala,ikawa na kwa muhasibu kuhesabu na vyovyote vingene
inavyokuwa alimradi ni kazi ya mtu ameichagua,pengine kazi zote ni sawa
kutokana na mahitaji ya mtu mwenyewe,imekuwa ni kwa kasi kubwa wale wasomi
kutaka kazi tena zenye mishahara minono,hiyo ikiwa wametoka shuleni,wao wakidai
wamepoteza muda mwingi wakiutumia kusoma sio kama vile wale waliobaki wakiamua
kutafuta maisha yao katika namna wanavyoweza.na wao wanafanikiwa zaidi,hivyo
ikawa isilete lawama kwa kuwa kama ni shule mtu umeamua kwenda mwenyewe,tena
kama ni chanda kilikuwa kikicheza tu ni lazima tutafute namna ya walivyokuwa
wanamchezesha,maana wengine wamejifunza vizuri ru.
Pengine leo hii utaambiwa sio haki yako,pengine ni
wito,mwalimu anayeamua kufundisha kuanzia saa moja asubui hadi jioni huyo
ametimiza wito wake,kwa maana ametaka watu kuelewa zaidi ya kile anachoridhika
nacho,baba wa taifa alipata kuridhika na mali alizonazo na kama angegoma
kufundisha watanzania mpaka sasa tungekuwa tunatawaliwa na mtindo tofauti
sana,pengine hata tusingepata nafasi ya kugoma,tusifananishe maisha yetu ya
kuwa hatuna uwezo wa kupigiwa simu saa nane za usiku kana kwamba kuna
mwanafunzi amezidiwa kwa kuwa kesho na mtihani,kazi ni kufundisha,swala la
kuelewa hilo hatuwezi kulazimishana..
Pengine ndugu zetu tuangalie na usalama wa nchi yetu,hata
kama tunadai haki zetu.haya mengine machache tu na ikiwa umeona umeshindwa
kuishi wewe,hata watoto wako wataishi tu,labda ikiwa haina maana ya kujipanga
tena maana umeshachelewa,wengine tuendelee kukaza buti maana hili ni janga letu
sote,kama tutagoma kula chakula tulichopika wenyewe hapa yapasa kusafirisha njaa,
maana tusipoileta katika muda hata wa nyongeza,hapo tutaeleweka kama wanafunzi
maana swala ni kuishi.
No comments:
Post a Comment