Monday, October 8, 2012

JIULIZE...


Unaposhindwa kabisa ama kuweza pia ni kheri ukajiuliza,jiulize kama ni kweli unahitaji mafanikio ambayo yatakukidhi,ukiwa na akili timamu,ukiwa na akili zako unazozifahamu,isieleweke kuzingulika kwani mwisho wa siku utajizingua mwenyewe,usiwe na haraka ya vitu usivyovifahamu,usiwe na  haja ya kutaka pasipo kufahamu,ikiwa kwako jiulize kama ipo kama kwangu,yako ni yako lakini ni katika usawa wa matendo,wacha niseme hivi ilivyo ikiwa katika kuelewa.

Angalia usije ukapotea maana na njia zimekuwa ni nyingi sana,anafatia na maswali ya kujiuliza unaweza kwama na kuoneka ulitungwa hadi  swali sijui jibu atakuwa nalo nani..kwani ingelikuwa ni kiulizo basi ni lazima ungenijibu wewe,mara nyingine gadhabu hutumika kwa kuona maswali magumu yakikusonga,mara nyingine maswali huwa marahisi ikawa unayefanya magumu jiulize mepesi yapi?maana swali la mtihani jepesi si ya kuwa umelipatia maksi..

Nilijiuliza nikasema sina haja ya kuuongelea mtihani labda iwe katika chumba chake,nikajiuliza yajana niliyoyaweza leo kumbe ni  mepesi,ndiyo maana nikawa najiuliza sana kuhusiana na siku ya kesho.utu uzima unamajina zaidi ya pesa ilivyo,maana mwanadamu haendani na fashion ingawa anaitengeneza mwenyewe,jiulize  kama shavu lako la kushoto liko sawa na la kulia,ili utakapopigwa hata la kulia ukageuzia na kushoto.

No comments:

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...