Wednesday, October 17, 2012

RADHI...

 
Ikiwa kwa yote yaliyopo, yaliyotokea,yalivyo ama kwa vile tu mtu unavyoweza kumfahamu mwenzako,kwa namna ya kusema na kumjua,ntaomba radhi pale ntakapoyakosea maisha yangu,sifa za kidunia ni jambo jema sana ya kuwa pengine umekuja kwa sababu iliyojengeka na hiyo,ntaomba radhi kwa wachache watakao soma na bila kuelewa kwa sababu kuna wale walioelewa,pengine hakuna maana ya kuelewa tofauti kama hujaelewa hapa ntaomba radhi tena kwa kuwa umeelewa tofauti,
 
 
Raha nyinngine jipe mwenyewe,makosa mengine tatua mwenyewe,wanadamu hawana dogo maana hata ikiwa katika usafiri kuna kubanana na kukanyagana wao watataka radhi,hapa pengine ukiwa na majibu yako kwa kuwa haukuomba radhi mapema na si kwamba ulikosea,bali ni katika namna ya utofauti,kwani unaweza kwenda polini kumkamata simba ili kumfuga naye akakudhuru tena bila radhi kwa sababu ameelewa tofauti nini maana ya adui,radhi si kwa ajili ya kujeruhi tu,hata kwa kuona kwamba imetokea,hapo ukihusisha muda pekee.
 
 
Muda mwingine ni wazi machache hayastahiri kutokea,dunia imeumbika kwa kusema yote ni mazuri na ilikuwa hakuna haja ya kuomba radhi kwa kuwa mti mzuri hutoa matunda mazuri pengine uwe tasa.na kama kuna utasa basi itapasa kuomba radhi kwa kutokufahamika,zaidi maisha yaendelee kwa kuwa kuna mengi ya baadhi ambayo yanaweza kukuletea hadhi.

No comments:

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...