Vitu vinavyokuja kirahisi mbele yetu kama zawadi inaweza
kukupelekea katika sehemu nyingi chagua na kuwa na uzuri katika kila jambo, amua kutoka ndani ya mfuko
wa moyo wako na kuangalia nini unataka kufanya katika maisha yako ukitakiwa kuyandeleza maono na
mawazo yako.
Usijifiche bali fanya ni lazima kufanyia kazi kipawa chako ikiwa ni
nguvu na tabia ya mtu, amua kwamba utajisukuma ili kufika mahali Fulani kwa
nguvu zako mwenyewe,
Nguvu ya mwanadamu ni kubwa sana Zaidi ya ufikirivyo kile
ulichoamua hakuna mtu awezaye kukukataza, anza kuongeza na kuimalisha malengo
yako kwani mafanikio unayachungulia unayachagua wewe mwenyewe na kipaji chako kikufikishe
pale.
Kila siku yakupasa kutafuta nini njia ambayo utafika siku na
watu wakuulize na washangae umefikaje pale, maisha yanaweza kuwa ni silaha kwa
muda mwingine na vitu vingine watu hawafundishwi hivyo sio kila kile ufanyacho
ni mafanikio yakupasa kuwa na nguvu zaidi ya maisha yako yenyewe na namna
unavyoyapima mafanikio binafsi, kubali kwamba kuna watu wanaitafuta iyo nafasi
uliyonayo,
Hakikisha unatumia siku yako vyema haijalishi ukiwa na furaha ama
chukizo yakupasa kutambua kuwa ni wewe upo katika hiyo hali na nini kifanyike,ukiwa
unajua unachokifanya haikupasi kuwa na maisha ya katikati inakupasa kuvuka
vizuizi, usijaribu kuacha kupigana na kukata tamaa, jiamini na Pigania Maisha sio
leo wala kesho Kwani umekuja kuishi.
Tambua uko katika misheni ambayo inahitaji ukamilisho
wako, usijikatae kwa kukosea maana wengi waliofanikiwa wamekosea sana, utajifunza
kutokana na makosa bila kujali ni makosa ya aina gani maana mwenye makosa
ndiye anayetegemewa kufanikiwa, sema ndiyo kwa kila jambo linalohitaji kuendelea mbele, jaribu unapopata wewe ni lazima utambue
kuwa kuna nafasi nyingine katika maisha,
Kwa kile utakacho toa ndiyo hicho
utaingiza, usirudi nyuma kamwe muda wa kushindwa ulishapita,kipindi kigumu huwa kinapoteza vipaji vya watu
wengi na kujikuta wakibaki wakilalama na kufanya hakuna, funguo ya kufanikiwa ni
kujiamini kujifunza na kutenda kupitia makosa hayo hayo,
Toa sadaka yako leo kwa
ajili ya kesho nzuri inayokuja na utumie ubongo wako vizuri ili kukuendesha kuwa na furaha
na mafanikio unayoyategemea.
No comments:
Post a Comment