Tuesday, November 13, 2012

RIDHIKI NI POPOTE...


Ridhika katika kufanya maisha yako yawe unavyotaka,maana nikasema mazuri pengine ndiyo mabaya kwa kulinganisha na yale mazuri ya wengine,maisha hayajawa mpira mpaka ikaja kuyapiga ikiwa kama dana dana,shida yapasa mtu kuzipata peke yako,ridhiki ikiwa yako haina unyang’anyi kwani kwa kile ulichokiandaa ndiyo hicho kitapendezea kulika,kuweka mezani chakula si kwamba ule hadi meza,maana njaa lazima itakuja,ikiwa kama ni ridhiki lazima chakula kitaandalika tena na endapo itakutwa meza haipo itastahiri kulika mpaka sahani zenyewe.

Maisha hayajawa mchanga mpaka yakafika namna ya kuchanganya watu pasipo kuelewa nini cha kufanya,wengi wakiwa wanatafuta ridhiki wakiamini pesa ndiyo tatizo la kulitatua tatizo husika pekee,ukiamini endapo ukiwa una pesa yote yanaweza kurudi mwanzo,ikiwa ni njaa,sahani Pamoja na meza yenyewe.maana unaweza kutokudhani baadaye kwa kutokujua unataka nini.ridhiki yako ikawa kama ni mnyororo uliojifunga maana hakuna wa kumuuliza nani aliyefunga.

Ridhiki haiokotwi bali inatafutwa,yakiwa saba bora kuchagua lile la mwisho maana usije kuridhika na moja wakati haba lipo,haipaswi kuchukia na hoja moja wakati ya wengine yanaonekana kama vioja,yaweza kuwa yako,unaweza kuwa wewe.ridhiki haimfuati mtu,ridhiki haichagui kabila wala mahala,ridhiki huenda pale kwake kuliko na usahihi,mwanadamu anapaswa kuwa makini ili kuelewa popote yake,ikiwa kama mdomo umekosa ridhiki kwa  kula basi hata pua zitanusa,pengine masikio yakasikia lile lililosemeka na vingine vikawa vile vilivyoungika.

NENDA UKIJIAMINI KATIKA MWELEKEO WA NDOTO ZAKO..ISHI MAISHA YALE ULIYOKUWA/UNAYO YAFIKIRIA.

No comments:

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...