Wednesday, August 15, 2012

NAMNA(2).

Katika kufanya ni kufanya yale yanayoendana na kile kinachoendana na maisha yako,ikiwa maisha yanahitaji uvumilivu wa maelfu ya muda,kuna namna ya vile unaweza kujiuliza ni namna gani unaweza kufanya  maisha yako yakaonekana na mtazamo bora ikiwa yameonekana yanatakiwa kurekebishwa,pengine ni katika mapenzi ama vile ilivyo katika hali ya kuuboresha mwili,wachache wakiwa wanafaidi kwa migongo ya wengi,na hii ikiwa wengi wetu ni hatujitambui,ingawa kila siku tunazungumza maswala ya kujitambua na bila ya kuelewa ni kujitambua katika namna ipi?

Leo imefika usikubari kuwa mzigo,pengine ikiwa utabebwa sana tena vibaya maana na mbebaji akiwa amechoka yu radhi kuutupa mzigo wenyewe,ikiwa hakuna namna ya kuweza kusema maisha ni marahisi kwa sasa,basi ni kuyapokea kwa utambuzi  wa kufanya  na kupokea kile ambacho mtu amekiamua kupitia fikra zake mwenyewe,pengine ukawa  hausikilizani kwa sababu ya kufanya kwako ni tofauti tena bila ya kujua unaweza kutoa lawama,na bila kujilaumu mwenyewe.

Hakuna Yule asiye na kitu,maana hata katika mawazo,swala ni utofauti ambao kila mtu anajitahidi katika kufikisha maisha yake mahala husika,unapotaka kufika mahala fulani hapo ni lazima utambue mahala ulipo,ikiwa na watu zingatio wanaotakiwa kujitambua ni tofauti,kawaida ya malengo huja baada ya kufanya yale unayoyatambua,hivyo ikaja wakati tumefanya tofauti hiyo ni namna ya kujitambua tofauti,pengine hata   mtu ukafanya ukaeleweka kufanya tofauti na jinsi ilivyo.

No comments:

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...