Saturday, May 5, 2012

MATEMBEZI


tuwaze vile vinavyofanya kutembea na sio vile vinavyofanya kutembea kutembeza
sio kwa ubinadamu tutafikiri labda ni kwa kupanga maneno,
ikiwa kwa moja iliyokubwa ndiyo huwa mwongozo,
katika kuongoza hapa kuna mbinu tofauti pengine kwa walio na hitaji la kupigana vita ya kuwa si matusi zaidi ya kumfanya mtu kuelewa,
maana wewe ndiyo unakuwa mwalimu,au mpiganaji..
pengine mwalimu hajui zaidi ya mpiganaji
hapa tutafikiri maana,

pengine ni kurejesha viumbe duniani ikiwa tunasema tutazaliwa mara ya pili maana ingalikuwa ni zamu ya mtu wa mwaka mwingine basi tungekuwa tunachelewa sana,
ikifahamika kwa wengine mwisho wa dunia ulishatakiwa kufika,
hapa kuamini,
ikiwa lengo ni kutaka kweli kutembeza,
pengine tusijari mwendo zaidi ya kufika,
maana kama itaeleweka safari ulianza zamani basi kuna uwalakini wa kuitwa na mwenfo pole,
maana tukijaribu kupunguza kasi ya maneno hapo tutakuwa tunapunguza uwingi,bora yakawe maneno yote na huo upole pia,
simba haelekezwi na swala kumkamata twiga,
bali ukaribu wa simba na swala ni zaidi ya vile wa twiga,
maana twiga yaweza kuwa ni mtamu au basi yu mrembo na urefu wake na ikawe nyama ya baadaye,
wale twiga wafupi ndiyo wale warefu wa wenzao.

tutatengeneza vingi na tukajua ni vile vile,
wazee wa zamani wanafikra ya kuwa na uzoefu wa maisha
kijana wa sasa anatakiwa awe na fikra ili kuweza kupingana na shindo za maisha,
hapa fikra ipi sasa huwa ya kijana na mzee,
na hapa ndiyo maana na kuweza kifikiri,
yaani isingelikuwa hivi basi siyo maana ya kuwa vile maana sio lazima,,
pale mtu atakuwa na fikra,
pengine imani,
ieleweke sio dini,
kwani hata tukaulizwa dini ni nini tutasema ni imani bila ya kuifahamu imani yenyewe,
pengine sisi hizo sio dini zetu,
ni imani zetu...
pengine sisi ni imani zetu na wengine sio dini zao,..

hapa ni kuwa mahala kote maana unaweza kutokuelewa bila kufikiri,
yaani hamsini hamsini,bila ya kumalizia na mia
maana hilo ni jibu baada ya kutembea
yule anayetumia imani kufikiri ni baada ya ubongo,
maana ubongo ni kuwasilisha..
basi tukafikiri kutengeneza roboti bila ya kujua tutawaundia nini,
maana hata tusiwaze kutembeza,,
si watakuwa kidogo kidogo..
watatubeba wale..

imefika wakati tunataka kutembeza vile visivyotembezeka,
maana kama utamtembeza mtoto mchanga ni sawa na kutembeza roboti la umeme kwa nguvu,
hapo nguvu imesema.
tena kama ni umeme unatembeza si nyepesi kwa mwanadamu kutembeza,
maana si tungetembeza!!
hapa tusimfikirie mungu sana labda kila mtu awe na fikra zake,
hii itasaidia sana katika kutembeza maisha,,
pengine maisha hatujayafikiria sisi tu,
walivyoanza wazee sidhani kama tuliwauliza japo hata kuwasikia wakisema,
kama walikuwa wakimya jaribu kujiuliza maana ndiyo kukua na maswali,
ili kuweza mtihani inakuwa vyema kwa kujiandaaa,
tutajiandaaje bila maswali?

kweli yapasa tujipe maswali,
tena mengine tuwasaidie na wengine,
pale tu tunalipolizika na maksi zetu
ikiwa na mshindo basi tutembee tuyaone kwani macho hayasemi mma..

By:Benson G.Makaya

No comments:

ELEWA 2

  Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye na kukataa kuelekea hata kwa ku...