Saturday, May 5, 2012

SAHIHI...


Sahihi ni namna,sahihi ni kitu,sahihi ni uwezo,sahihi ni hali,sahihi ni neno linaloleta maana.
yaweza kuwa maana ipo lakini ikawa sio sahihi,ili isiwe sio sahihi yapasa kusahihishika,
ingawa na yenyewe ni maana,wanaosahihishika sio wakosaji,
ni wale wanaotaka kusahihisha,pengine wanafanya sahihi,au wameona sahihi au hata wao wakawa sahihi.

Tunapozituliza nafsi,ikiwa na kichwa kwa ujumla ni lazima kuwa sahihi,
 katika yale yaliyosemeka mwanzo,ikiwa kama ni kitu basi kieleweke kuwa sahihi,
maana ubovu nao unakuwepo na usahihi wake,ikiwa mmoja akafikiri sahihi zaidi ya mwingine kwa upande ulio wake,sahihi huja katika matokeo ya maswali ya kuwa  maswali huwa sahihi,
pengine tukikaa kimya tunakuwa tunafikiria lakini sio sahihi zaidi ya swali linapokuja kama unafikiria nini,
 pengine tuingie ndani zaidi,ikiwa tumetaka kuujua usahihi.

Siyo usahihi wa makosa wakati bado hatujafa,maana mengine bado hayajatendeka,
 kama mtu kalenga kukosea ni si vile afikiriavyo aliyepatia,
maana kama kuinama ni sahihi basi watu wengi wasingesimama,
tena tungebaki na haja zetu bila ya kuonekana ni sahihi endapo tukataka kusimama,
hapa tufanye sahihi ilivyo katika umbo na hali ndiyo usahihi wenyewe.

Usahihi sio kama swali limekuja mwanzo,kumbe bora sahihi kuliko swali,
maana kama kuna kujibu kwa wakati huu ni lazima kufikiri kuhusu usahihi,usahihi ni baada ya mtihani,
mtihani ni maswali au swali linaloweza kukupa usahihi,maswali yapo mengi sana,yote ni sahihi kwani yana majibu yake.

Katika kufikiri lile moja mengine mengi huja ndani yake,pale ndipo usahihi unapopotea,
tena siyo kupotea zaidi ni kujificha,maana kile kinachogombaniwa na wengi ndilo swali hilo,
hapo ikiwa kila mtu anataka kuweka ama kuleta usahihi wake,
yaani majibu..na baada ya majibu ndiyo huja usahihi.sahihi ya mwanzo ndiyo halisi ya mwisho na ndiyo maana kukawa na mwalimu,yeye akajua,akafikiria,akaweka..

Pengine na akadanganye kabisa lakini kwa mwanafunzi hilo ndilo jibu sahihi.Tuyaache maswali sahihi yaje maana majibu yapo mengi sana,tena tutayajibu kutokana na vile mavazi yetu sahihi yalivyo,
hili ni kama swali maana usahihi unategemewa na wewe.

No comments:

ELEWA 2

  Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye na kukataa kuelekea hata kwa ku...