Tuesday, July 31, 2012

MAKOSA..


Machache yanakuwa ni ya kila mtu zaidi ya mwengine aliyonayo,maana kuna kusikia ikiwa mmoja amefanya tofauti,namna ya kusema ilivyo na kufanya huwa mbaya zaidi ya watu vile wanavyosema,ikiwa kiti cha mtu mmoja ni makosa kukaliwa na watu wawili,hapo baadaye tukaja na kuambiana ilibidi kufanya hivyo baada ya maongezi,na bila kudhani kabla mapema kama maongezi hayakuwepo.kumbe siyo lazima mmoja kuona vile walivyoona wengine,hata katika upande wako jua hayo ni ya kwako tu.

Ni makosa sana kumfundisha mtoto maswala ya kikubwa,ni makosa sana hata kumwona mtoto akifanya mambo ya kikubwa,pengine hapa tumeshindwa kuambiana ya kitoto ni yapi,na ya kikubwa ni yapi.pengine na watu hao wakafahamike bila ya heshima ya umri maana na yenyewe imeleta ukubwa,kuna wakubwa wanamambo ya kitoto na hayo ni makosa makubwa,pengine kwa upande wangu,labda na watoto waachwe watende makubwa.

Inasemeka katika makosa ni namna ya kuweza kufanikiwa,na wanofanikiwa ni wote ikiwa ni watoto na wakubwa,mafanikio hayana umri,pengine ndiyo maana mwanadamu anaweza kufanikiwa katika umri wowote,hii ikiwa kama atachelewa sana basi kuna makosa aliyafanya,pengine ni mipango tu.makosa sio ya kumfaya mtu kukata tamaa ya maisha kwani ndiyo nguzo ya kufanikiwa,hata mwanadamu asifanikiwe bila makosa,tunaweza kukosa vingi ikiwa ni pamoja na pesa,afya na yetu mahitaji mengineyo.tukubari kukosa pale inapotokea ikiwa ni nafasi pekee katika kuelekea kufanikiwa,lakini pale tunapojifunza kweli.

No comments:

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...