Kwa muda mwingine huwa nawaza niandike nini lakini kwa
sababu zingine huwa nawaza kwa nini sababu za nini?maana mengi ya duniani ndiyo
ya vinywani,mengi yakusemeka,mengi ya duniani ndiyo yale kawa maandishi,pengine
tukajua huko.pengine tukaona ni nini kipo huko,tukisema sasa tumerudi hapo
tutaulizwa tulikuwa wapi,hapa tuweke sababu,hapa tudanganye tena
ikaaminike,isije aminika ya kuwa ndivyo ilivyo bali iaminike ya kuwa ndivyo
ulivyo,sio kutafuta ni kufanya,sio kufanya ikaeleweka,sio kueleweka ikawa
imetafutika,hapo sababu zitakuwa nyingi
sana,hapo tutashindwa kujiuliza na kujiuliza na kujipa majibu,tena ndiyo
haswa tueleweke kama hatujaelewa kwa maaana ya kushindwa tena labda hatukusoma vizuri ama yalikuwa tu hayaeleweki kwa
kubisha,sisi wengine ni wabishi sana,sisi wengine ni watata sana,hata kama
maneno yanafanana,kwa machache lazima kuelewana.
Muda hauji ukaja
ukasema,muda unasema wenyewe kwani ni lugha nyingine pengine wakaelewe wale
waizungumzayo lugha hiyo,katika kujifunza kuna kujua endapo mtu amefahamu,akiwa
amejua au hata amehitaji kutambua,najua tumechoka sana,pengine tukiwa
tunahitaji lakulifahamu kulingana na huo muda,pengine ni sisi wenyewe wa
kujifahamu maana hata huo muda ukawa hauna maana,kwa kuwa mdogo ama kupungua
katika yale yanayotakikana
Hakuna mtu anayependa kuchelewa kama sio kuwahi sana.pengine
watu wameshangaa kuona mwezi wakati wengine wakiwa na hitaji la
jua,wakilitafuta kwanilinasikika tu,wengine wachache walilliona wale tunawaita
wazee tena wazamani maana siku hizi kuna wazee wakisasa,hapa sijui
tuliuchelewa muda ama tuliona tofauti,au
pengine ndiyo namna halisi ya ilivyo..ilivyo maana na namna ya mtu akatambue
akaishi vipi,ilikupata moja lazima kufikiri na mwisho,kwani sio tatu pekee ni
bora,hata kumi pale ikawa bahati nasibu.na hapa watu wanabahatisha sana na
kusema wameweza,hiyo ikiwa ni imani ya kutaka kuweza na kushindwa.
Mwisho wa kumalizia ndiyo mwanzo wa jambo,ikiwa tu
limeonekana,limesikika hapo kutakuwa na mwisho na mwanzo tusiufahamu,tena
tukasema kwa yale tunayoyafahamu na kuyaweka kweli,hapa huwa tunaongea
sana,huwa tunajiona tumeweza tusipojua hitaji ni tofauti maana tusingeweza
kuwaza pamoja,hapa isinge kuja ile namba moja,ikiwa hivyo tunahitaji
umoja,maana kwa umbali tusijifanye zaidi hata tukasikilizana,hapa lengo ni
kuelewana,kwani hata ingekuwa namba zinajipanga zenyewe sidhani kama mbili
ingependa kukaa nyuma ya moja na wakati yenyewe ni kubwa,fikiri kuwa na nyumba
mbili na mija pale unapohitaji,pale unapokuwa na kitu chako kimoja fikiri mbili
kuwapo kama si furaha ndani yake,labda isivyo amani kwa yale mabaya kwa
mwengine.tumalize kwa kumaliza.
No comments:
Post a Comment