Haya yangu
Tanzania isiwe ni nchi ya kulalama,eti tukataka kufanya kwa
kusema ni haki,pengine kila mtu yapasa kufahamu haki yake,haina maana ya kuumia
na kulalama kwa nini umeumia,hapo hatutatumia udikteta,hapo hatutafanya
maonevu,pengine kwa yaliyo machache tusifanye roho zetu zikawa siasa,hapa
lazima tuelewe siasa ni nini,maana kwa pengine jana ikatokea mtoto wa jirani
amejikwaa basi utasikia chama chao hao,kesho ikija tunasema aaah hawa watakuwa
wamelipizia,tukiwa tunaenda na kusema tunajengea watoto wetu maisha,hapa
tutakuwa tunajijengea makaburi kwa bila ya taarifa,maana wengine wataona haina
haja hata ya kukuzika,watachoma moto tu.
Kesho jamani ije bila ya kutokusahau,maana mengine wamekuja
leo wakiwa wameumia sana.tufikiri hapo mwanzo kama tulikuwa hatulimi,leo hii
tunaambiwa ni kilimo kwanza,ni kweli hata iliposikika,inaleta maana ya kuwa
imemlenga Yule anayeambiwa,maana hata mtu ukakubari ndiyo lazima tufahamu
kwamba kesho itatokea lake,wengine hawana hata kazi,eti tunasema hawaja
soma,hawa wengine waliosoma ndio wanapigwa ili kuonyesha haki,nani apigane?maana
mwenye haki asiyesoma,mimi yangu haya mwenzangu na mimi sijui haki yako iko
wapi,tena angalia usije zikwa mzima.
Pengine nchi yetu imekuwa tambala bovu linalongoja matope
yaje ilki kuyazoa,yakija masafi si wanasafisha wenyewe,tena huwa si vurugu
kwani huitwa ruzuku,wanagawana wachache tu,wasichoke wengine kutupa
msaada,wachoke wengine wenye kumaliza misaada,maana imetokea mkubwa kajua kama
mkubwa kajua unadhani patakalika?
Haki yangu nitaifurahia mwenyewe,haki yangu haipaswi kwenda
kama kifaranga na mwewe,leo isiwe lakini kesho itakuwa,haya ni yangu yamependezwa
ingawa tunaangamizwa,kubali mdogo ndiyo wakubwa walivyotufundisha,kubali mkubwa
ndiyo wadogo wanachostahiri,chukua chako ondoka,maana vengine vya wengine,
Haya zenu jamani...!!
No comments:
Post a Comment