Sunday, July 15, 2012

MBISHI.

Mbishi ndiyo huyu huyu unayempa heshima kila siku,tena wapo wengi,kwa maana ukaamke asubuhi na kuandaa heshima zao,hapo katika heshima wale wanaobisha huwa ni wakubwa,hata katika kubisha ikiwa katika hali ya kawaida kwani ukifiri haina maana ya kuwepo mkubwa na mtoto,haina maana ya kuwepo heshima,maana kama ulijitolea nguvu zako kuwalisha watoto wako na sasa ukabisha kwa kuwa na matendo yasiyoendana na ulimwengu  basi utakuwa umebisha mwenyewe,na hivyo ni lazima upokee lawama kwa hao uliowazidi,maana wao hawajui kitu,labda vile watoto wanaelewa kwa namna ya vile ilivyo,mkubwa akabisha kwa namna ya kujua kile cha utoto.huku akijua chake.

Mara nyingine watu wengi hufikiri nafsi za watu kama za kwao,hawaelewi kama kubisha kwao ndiyo nafsi za watu wengine,wabishi wanaweza kukufanya hata kufa,kwani ukifikiri kwa uwepo labda utakuwa unafahamu lakini kwa yaliyopo imeonekana ukibahatisha kwa kutokujua lile wanalobishia wabishi.maana mbishi akibisha amemaanisha kujua zaidi,kuwa mbishi ni vyema hasa katika maisha haya ya kisasa,lakini ni lazima ieleweke kama unayabishia nini,tena ikiwa kwa kuyaelewa.

Ubishi raha sana,ukiwa mbishi ni lazima uwe na kumbu kumbu ya kutosha,maana kesho itafika utaambiwa neno lile lile,ili kutaka kukutega,kuzunguka hakuna mwelekeo zaidi ya mzunguko,maana hata hiyo kulia na kushoto ndiyo inayoleta ubishi zaidi,dunia inazunguka na sio vile inaelekea kushoto ama kulia ama hapo utabishana ukiwa haujui kweli.

No comments:

ELEWA 2

  Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye na kukataa kuelekea hata kwa ku...