Sunday, July 15, 2012

MSEMEA MWENZA..!


Uwezo unatofatofautishwa zidi na yule  atendaye hivyo,sema wewe mwenzako bado hajaweza,eleza wewe ya mwenzako siyo ya kuyatenda,maana hapa tunataka kuona wewe,yaani uwezo..ndiyo ikiwa inahitajika namna ya kuonyesha kwamba ile ilikuwaje,katika mwanzo kuna mwisho,na isingekuwepo hata tusingetamani,maana si ingekuwa tofauti na sasa?pengine tutamani wenzetu wanavyosema,ikiwa ni kutaka kukuza uwezo wako,lakini tukisema yao tutaonekana wambeya,pengine wengine wanafanya yao tuseme,ama tunajisemea tuu,na endapo ikifika wakati itaonekana   tumeshindwa ni kwa sababu hatukusema yetu.

Hapa anatafutwa Yule ambaye amemsemea mwenzake,maana katika kipindi cha kuonekana kusema hakuonekana msemaji na baadaye ikaja bila ya kuelewa,pengine ni nafasi yetu,mwengine ni nafasi yake,haina maana ya kuomba ruhusa wakati hatuna hitaji nalo,tena isiwe tunatega,isieleke namna ya ilivyo mtego ikawa ni kama ombi,hapa na pengine yatupasa kuelewa.

Sema mwenyewe maana hakuna wa kukufanyia,fanya kwa nguvu kwani ni nguvu zako zitakazo sema ,hapo kukiwa hakuna woga maana yamesikika mengi na hakuna kilichofanyika,hakuna yaliyotendeka kwani  wengine walidanganya,unaweza kufanya kwa nguvu lile lililo na uwongo hapo kushindwa kueleweka,maana hata wanaomsemea mwenzake wanasubiri neno ili  mradi limesemeka ili kuonekana wao wanaweza,tutajua linalofuata kwa matokeo yanayokuja,maana si tumechagua kusema wenyewe?
hapo labda tuseme ya kwetu maana kama yakiwa ya watu tutakuwa wa kwanza kwa kutokuya weza,fanya yako..


No comments:

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...