Ni kama pale tunapowapa watoto wetu usaidizi wa kuweza
kupata hesabu ali mradi wasikosee,hesabu hizi ni namna inayomfanya mwanafunzi
kuona kama anaweza,hiyo ikiwa kama mtihani maana haina haja ya kuhesabu kitu
bila lengo maalumu,tutaeleweka wehu kwa kuhesabu tu tena tutakuwa tunahesabu
ili iweje?maana katika hesabu kuna kutaka kugawanya,kutoa,kujumlisha,na
kuzidisha,na hii yote ikiwa inafanywa kwa hatua kwa hatua kwani kinachomaanisha
katika yote ni idadi baada ya kutoa hesabu hizo,labda leo tujiulize sijui tupo
wangapi katika nchi yetu,au haina maana ya kuwapo...?
Yaweza isiwe na maana ya kuwapo kwani tutahesabu nini wakati
pesa ya matumizi imeshatoka..?la msingi ni kuingia sokoni kwa namna iliyopo na
tutakavyo rudi navyo isije kuwa lawama,maana baadaye itaonekana kama watu
hawakuhesabu vizuri, ni kwa sababu mwalimu alishatoa majibu yake mapema kumbe
naye alikosea,kwani hakupiga mahesabu kwa yaliyopo,maana kama tutakosea kwa
yaliyopo haina haja ya kufanya hesabu za mbele.
Wageni karibuni tu nyumbani chakula kipo,tumepewa pesa ya
matumizi nyingi na bila ya kujua nani atazitumia,hii ni hatari kwani imeonekana
hatukujua mtihani kama utakuwa na mahesabu ya kuzidisha,tutachanganyana sana
hapo mbeleni,maana yaweza mzawa kukosa kula ikiwa hata mgeni naye amejiandaa na
pesa zake huko alikotoka,tutalala njaa sana
na haina haja ya kulalama kwani tumeipokea vyema .
Hizi ni propaganda,tusiseme watu wamekuwa wazembe kwa kukosa
kula na maendeleo finyu, baada ya hesabu washindi wakionekana wengi hapo
tutajua nini cha kuwapa.
No comments:
Post a Comment