Maana bado inaendelea,hali kuwa ngumu.ikiwa kwa mara ya
kwanza tulipoambiwa tukajifanya tumeelewa tena sasa tunaambiwa turudie
tunashindwa kuelewa.tumekuwa bidhaa sasa mpaka tukashindwa kuzuia
upepo,tunapelekwapelekwa tu,hatuna misimamo zaidi ya kugombania
vyama,tunapumbazwa na sifa badala ya maisha yanayotuhusu,maana tunataka haki
pasipokujua haki tunapata wapi zaidi na badaye ije tumlaumu mtu,eti aahh Yule
hakuwa kiongozi bora,sasa tunataka nini,maisha bora,kiongozi bora,chama bora au wewe bora?hata
nisifahamu maana kila mtu ana kujifahamu mwenyewe.
Kesho tuangalie tusije gombana,maana hivi tunavyoenda bila
ya kuelewa hiyo inaashiria jambo bovu,maana tutaenda kinyume na maana ya mwongozo,hata kama ni mbovu.nzima ipi?hata hivyo hakutunga yeye..hamkujua ya kaisari anapaswa apewe nani?,sijui hata tutajengaje maana
kila mtu atataka kuujenga mnara wake,ili uwe wake ndiyo ndiyo hapo
tutatofautisha ujuzi na pesa,mwenye nguvu atajenga tu,kwani we hujui namna ya
kufyatua tofali?haina maana ya kuitwa mtanzania kama ni mchina.
Haina maana kumkataza mgeni asiingie na wakati ni
kwake,maana ameshanunua sasa tunataka kuwalipa mara mia au?mkubwa akielewa
amekosa sio kumchapa mkubwa mwenzake,leo tunaondoka bila taarifa,samahani hivi bunge la nyumbani litaongozwa na nani?kama mama
na baba wote wamechukia,na familia zenyewe zilivyo za kihindi kila mtu anataka
aonyeshe hasira zake,rudini bungeni jamani..swala la kukaa chini na kuangalia ni
nini kifanyike,maana tutagombea viti huku watu wanaendelea kuteseka,maana sijui mtueleze mnang’ang’ania
nini na wakati mnashindwa kusaidia watu walio katika msaada,hapa mahala hapata
kuwa sawa, hali bado inaashiria vigumu.
No comments:
Post a Comment