Wednesday, July 18, 2012

POLENI WATANZANIA..


 
Poleni watanzania,wabishi na mimi nimo..!!maana kwa misiba mingi kufikia,pengine wengine wanasema mungu ametoa na mungu ametwaa vile tukafarijiane majumbani kwetu,muda huu huu wengine tumechelewa kufika eneo la tukio japo tukarusha kamba kuwaokoa wachache pengine ilitakiwa kutokuruhusu leo na kuwa kesho lakini ndiyo imetokea,haya ni majonzi yetu,hapa tunastahiki kushtuka,maana si kwa kutokuwa kawaida bali kuwa tumeuweka uongozi pembeni na kuweka ubinadamu,maana fikiri unaambiwa mtoto wako yupo humo,pengine je wewe ungekuwemo humo?haya ni kiimani zaidi,haya ni ya mungu.


Tusife moyo kwani japo tunarekebishana kidogo,tukumbuke hiace zote zimeacha kutembea mijini na sijui ni kwa sababu ya udogo,ajali ama foleni,pengine bahari imekuwa na mabonde,na madeleva wameshindwa kuendesha kwani walizoea tambarale,pengine ni wazi inahitaji kuvichunguza vyombo vyetu,maana ndiyo tulivyonavyo na kama watu ni wengi inapaswa kuwabeba ikiwa watu hao wanashughuri za kimaendeleo pande ya pili

Zanzibar ni kwetu ndiyo maana tuliungana,kama ingekuwepo sasa ni mimi na wewe,katika muungano kuna mengi humo,mwisho tunapata undugu,kutoka dare s salaam mpaka Zanzibar sio mbali kwa ndege lakini tumezoea meli,na boti huu ni usafiri unaotukidhi na maisha yetu,hivyo tunahaki ya kuwa makini na vyombo tulivyonavyo,ikiwa kama vinataka kuzeeka basi tunavifanya virudi katika ujana kwa maana kikizeeka sana hatuna budi kununua vipya,poleni sana ndugu zangu,poleni sana watanzania wenzangu..
Mungu alaze roho za marehemu pema..!!

No comments:

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...