Huwa yanakuwa mazungumzo kwa kuwa aliyeleta habari alidai
kumaliza kutoa maelekezo,leo ukiwa unazungumza kwa kutaka kuhadithia habari
bila kujua hiyo ndiyo habari yenyewe,pengine ikawa ni taarifa kwa kuwa habari
yenyewe ni kama muhtasari,ukijaribu kuonja ni vigumu kuondoa ladha tumboni,labda
isingetangulia taarifa basi hakika ingekuja habari kamili ingawaje imeonekana
hakuna aliyesikiliza habari kwani baada ya habari kuisha mazungumzo yanaweza
yasiendane na habari.
Haki sawa kwa kila mwanajamii,haki si sawa kwa mtoto na
mkubwa,labda iwe umesikiliza tofauti na kuona mageuzi katika kichwa cha
habari,lakini mazungungumzo yaliyofika baada ya habari yameonekana ni habari
yenyewe.mengine hayapaswi kuyazungumzia humu maana wengi wao wamekuja kwa kasi
wakitaka japo kuelewa kichwa cha habari lakini wameonekana wataelewa habari
yote ikiwa bado umri hauruhusu.
Msomaji wa habari anapaswa kuwa kama daktari,maana kuna
mengine yametukia sasa hivi,kuna mgonjwa ameingia wodini baada ya daktari
kumaliza muda wake wa kazi,muda mwingine ni wa ziada,muda baada ya
kazi..ukifanya kazi muda baada ya kazi bado huitwa ni kazi lakini unakuwa
umejitahidi kwa kuzidisha muda,pengine ndiyo huwa ni kazi nzuri zaidi,pengine huwa
ni taarifa nzuri zaidi..ikiwa mtangazaji kamaliza habari labda atuletee
mazungumzo ili ijulikane baada ya habari nini kifuate ama kilifuata.
No comments:
Post a Comment