Monday, October 29, 2012

SIMAMA...


Haitakuwa njema kwa kuokota bila ya kumfikiria Yule aliyedondosha,haitakuwa na maana ya kuinama bila ya kuangalia pale utakaposimama,leo ikiwa inazungumziwa sana ni lazima kuifikiria kesho itakujaje,yamekuwa magumu sana kwa kulinganisha namna za kufanya,yaani mambo huja kwa kuwa yana njia zake,ikiwa kitu kimedondoshwa kisije bahati ya kuwa umeokota,mara hapo ikafanana na namna ya vidude vilivyo ama ndiyo bahati zilivyo,fikiri endapo utasimama na kukuta umeokota mke,maana ndiyo bahati yenyewe.

Usipojua leo ule nini kesho huja na kukufanya  ushindwe kula hata maini,nimeona mengi..umeona mengi,,ikiwa unamsemea mwenzako ana nini fikiri ya kuwa umefanya nini,fikiri endapo umefanya nini ni sawa na kesho ikaja na yako yakawa kama maini,maisha ni mapambano..maisha ni kusimama vijana wakisema kidete,kwa imani yenye msimamo ndiyo kuweza kufanya vitu vilivyo simama,hakika haina haja ya kifikiri wakati hauna uwezo wa kusimama,japo  kiakili.

Usiogope ya  mtaani kwa kuwa bado hujasimama,usiombe samahani kwa kusema kana kwamba unataka kusimama,labda kwa waliokuwa wamesimama wakae,ama kwa ilivyo kusimama na kuwaziba walio mbele,hakuna anayeweza kukueleza yale unayoyataka ikiwa yamesimama katika fikra zako,pengine ukielewa tofauti ya jambo yapasa kusimamia lengo na kueleza Mawazo yako.

No comments:

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...