Thursday, October 18, 2012

NAFASI YANGU ILIPO.


Kama nikianza na kupanga mstari kwa kuwa ni foleni baadaye ntajikuta nipo pale pale tu ikiwa kuna uvumilivu wa kile kilichotakiwa kufanyika maana kwa muda kumepelekea machache kusemeka na kuonekana ni bora , bila mshangao imehitajika kitu cha kunyooshea ili kuunyosha mstari angalau wa pili naye akafuatia humo humo, maana kwa kawaida ya foleni wengine watataka kutanua ikiwa wana uchukuzi wa nafasi ndogo wakizifuata njia ama nia.

Jaribu kuamini kama unapopita mguu wa kushoto na wa kulia unapita humo, pengine yasiwe madharau kwa waliojisahau maana hawakupaswa kupita huko ulipopita zaidi ya kujua umepitaje, ukiwa mwalimu,ukiwa mwanafunzi maana hawa watu wanahitaji kurandana, ingawaje siyo lazima sana kwani nafasi nyingine wanapaswa kupewa wasiojiweza.

Lugha hii ikichanganywa na nyengine unapata wengine tofauti maana utakuja wakati na kusema umejileta ,kwa kuwa kile kilichoonekana sasa hivi yapasa kujua ndani yake kuna nini Kama vile leo inavyokuwa ni mkopo na kesho ni siku ya kulipa deni lakini unaweza kwenda ‘tena’ baada ya kusamehewa deni na zaidi  kukopa tena, madeni yanapokuwa mengi unajileta na kujisogeza kwenye mtego wa kuichanganya nafasi yako kuchanganyana na ya kule usiyoyategemea.

No comments:

ELEWA 2

  Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye na kukataa kuelekea hata kwa ku...