Inapofika wakati kitu kimeharibika huwa inaleta matatizo katika mazingira hasa ni kutokana na kutokutegemea kwamba kama zama za sasa si kama zile za zamani,ni wazi
nimekubali tekinolojia,ni wazi nimekubali mabadiliko Ni technologia,ikiwa nataka kubadilika na
kwenda na mambo ya kisasa,ali mradi ieleweke na ijulikane kama kuna uwezekano
wa kufanyika kwa jambo,isiwe imepitiliza kwa kuwa Wakati mambo yaliyotendeka yalitokana Na kile kinachofanyika zama za mda wako huu.
Imekuja kipindi sasa najenga uchumi wa mwenzangu bila ya kujijua,maisha yangu
nimeyafanya bidhaa ya bei rahisi ni si kama zile za kwake anazozitengeneza
kwake,maana nimeletewa mng’ao ili nijue kinapendeza,najenga huku nabomoa na
ifikapo kipindi najua kutakua hakuna namna ya kuona tena mbele kwa kushikwa
akili na mwanga wa vile vinavyong’aa kupotea,pengine kuongezeka umaarufu katika
hitirafu,ikiwa nimeruhusiwa kuwa dereva wa maisha yangu.haki taifa linapotea
kwa kile kidogo cha zama za leo,maana kila mtu anaminya jicho moja
anakuangalia na anafungua la pili
anakula vyake.
Zama za sasa inaonekana ni wazi vyakula vimepungua,ardhi
wanalima wageni maana wenyeji mmelima sana.tena mara ya kwanza walikuwa
wakilima na kujenga,labda ndiyo wanaanza kujenga tena.maana katika maamuzi ya
kiongozi mmoja yanaweza kukupa uhuru kama yanavyowaza kukupa vita na kukunyima
amani kwa kiongozi huyo huyo,hapa ikiwa tujiongoze,zama za sasa ni za ukweli na
uwazi,hizi ni zama zako
No comments:
Post a Comment