Eti kuwaza sana ni vibaya,nawaza sana nakuwa na mawazo nawaza sana yaliyo mema nawaza sana kuongeza kupata maisha sio kama ya fulani bali yale niliyoyawazia,wakati mengine yanapita Shukrani kwa muumba hazitaweza pita,Mwisho wa kuwaza unaelewa mwenyewe maana sio uwaze tu hata yasiyo na majibu,
Mbaya katika mtihani ni kuanza na swali gumu kuliko yote kumi utajikuta umefeli na kuyashagaa matokeo yakakupa mawazo tofauti yakuwa kabla ya kuingia katika mtihani uliwaza ukitoka utakuwa na mawazo tofauti zaidi ya yale uliyo kuwa nayo sasa,sijui niwaze nini nikufurahishe, nakusema siwezi ogopa ila muda haumdanganyi mwamuzi labda anayeamua akaamue.
Hivyo unachagua wewe,chagua wewe kuwaza nini mengine ni mazuri asikwambie mtu mawazo mabaya,ni kheri akakuongezee kwenye huo ubaya maana hata moto anaoupata yule anayechomelea na yule anayekaanga viazi ni tofauti nawaza tu,ukitaka kutokuwaza fanya starehe,ukifanya za kutosha na hautakuwa na mawazo ya kutosha,naposema starehe kila mmoja anayo katika mawazo yake unawaza kufanya starehe gani nasema hivyo maana kuna kauli inasema maisha ni mafupi sana hivyo inakupasa kuishi kwa thamani,matumizi yako yakaendane na mawazo yako ila pindi unapowaza kinyume huna budi kuwaza yaliyofanyika maana huo hua ni mwanzo wa mmomonyoko wa yale yanayofuata.
ukiwa unawaza yanayofuata ukawa hujui hasara yake maana kwa muda huo yanakuwa hayana mashiko na mmiliki yaani wewe uliyestarehe kwa mawazo yako kabla hujawaza sasa iliyopo ambayo ni baadaye.
Sikuwaza umri ni kama haya makubwa ninayoyawaza,wala kuna mengine sijawaza lakini yamekuja katika haya,mawazo ukiyaamini,yanakuletea imani yako inachokiwaza hata ukajiandae na utofauti ili kutokuyazidisha yaliyopo,maana nawaza sikufika hapa kama nilivyo wala sikuwa mimi kama nilivyo,sio tu kwa sababu ya nini ama fulani nikiwaza kwa mawazo yangu ni imani maana sikuijua kesho zaidi ya yule aliyeniambia niache kufanya ya kesho kwa kuwa hata usiku wa leo hayajafanyika.

Unapoona mengi kuna mengine yanakuwa sio makubwa yaliyowazwa zaidi ya kuonwa ikiwepo vingine nawe ukawaze hivyo,nikikiona nakielewa zaidi maana nikikiwaza ntakuwa kama nakiona,shida pale nawaza nisichokiona ninapowaza cha kesho na leo sijaimaliza hapa huwa naamua kufanya lililopo bila ya kuchelewa.
Kuna kucheleweshwa lakini aliyewahi kawai kesho ujifunze kuamka mapema ili kuyawahi mawazo kingafu ,maana kama mawazo yanaingiliana basi hata matendo pia,unapokufa wakisema utakumbukwa wengi ni kwa matendo yako,mengine waliyoyawaza husahaurika ,kufa leo uache mazuri yaliyotokana na mawazo yako na iwe kwa faida yako.
Nawaza ni kheri nizeeke muda mwingine ntakuwa nimepita mengi,nisionekane tu kwa mtu anayeona aonavyo bali nikajifiche kwa vile waonavyo,nilikaa na kuanza kuandika haya nliwaza mmoja atawaza yale ni mawazo tu,lakini kwa jinsi navyoona hata yule asemaye naye anataka kuonekana na mawazo bora,kuna vitu Mwenyezi Mungu amekupa na mwengine hana,Kama unaweza kufanya chochote bora fanya katika ubora uwazavyo.

No comments:
Post a Comment