Ni wazi mandeleo ya mwananchi huletwa na nafsi yake
mwenyewe,hii ikiwa ni katika kuamua endapo kuna
jambo lifanyike ama la..na ikiwa imechagulika na ieleweke,maana
pengine ni kwa faida ya wananchi,na katika faida ni
lazima isiwe na kudanganya toto,na endapo imekuwa bila ya kufahamika basi hiyo
ni sahihi maana hata sisi wenyewe tunaishi kwa muda mfupi tu,na pengine kupitia
wengine yaweza kuwa ni kwa faida yao tu,maana kama unajijua unakaa kwa muda
mfupi ujenge ya nini?
Hapo kwenye kujenga yatasemeka mengi,maana kwa vingine ni
lazima kufikiri endapo kuna tegemezi na hiyo ikaeleweke kama ni la muda mfupi
ama kudumu,vinadumu vyote lakini si nafsi ya mtu mwenye mawazo mafupi,utanenepa
kwa kuwa unakula,utakula na usinenepe kwa kuwa haujaridhika,tena maswala ya
muda mfupi yakiwa yanakuchanganya.
Fikiri kwa muda mfupi ili kuweza kueleweka kwa kuwa wengi
wanataka majibu,usikurupuke ya kuwa muda ni mfupi ikaja ndiyo sababu,hata yale
yaliyofanyika ni namna ya kutaka sababu endapo yakauliziwa,kesho tutaendelea
kulalama kwani wale wa kwanza muda wao unaelekea kuisha,tungalikuwa na thamini
na yale yanayotutegemea,hakika hata muda
mfupi usingekuwa ni sababu.
No comments:
Post a Comment