Tumeyachagua wenyewe,hapa machache yameongeleka lakini
yasipigiwe vigeregere,
usiombe kusubiri,usiombe usubiri,
maana pengine mazoezi
yatakuwa makali sana kipindi hicho,
yataongezeka kwa kulingana na muda,pale
tukitaka kupumzika bila hitaji letu,
Tukataka kutulia na kupigiwa makelele
majumbani kwetu,
pengine tukiwa hatutaki usumbufu,
pengine sisi ni wasumbufu
sana,
hapa ni kuelewa,hasa kwa mmoja na mwenzake mwenye uelewa.
Yanayochagulika ndiyo hasa tuliamua kuyafanya,
maana hapo
baadaye tukasema ziikuwa ni ndoto,tena tusijue tumeota wapi na lini?
bali
tukafananisha si tunaijua jumamosi?ya kila mtu ndiyo iliyo ya kwake maana
pengine ilipogeuzwa ilifanyika kwa namna ya kugeuka,
pale itakapogeuzwa zaidi
itageuka na yenyewe,
maana muda unasema unataka kwenda na sisi ili na wenyewe
ufurahi,
pengine ndiyo maana tunahadhibiwa kwa kutokuwa na muda.
Hapa mengine yaliyochagulika yakawa ndiyo hayo yaliyopita,
si
kama imegeuka vilee..tumefikiri sasa bila kujua uzee wa mbao kabla ya
msasa,
tutazeeka sana,kama tutapigana na bila ya hamasa.
No comments:
Post a Comment