Saturday, June 9, 2012

HII KALI..

Maji ndiyo haya yanaitwa 'water',na 'man' sio neno bali ni kauli ya kuogopa,hapa tunataka uhai..hapa tunataka pumzi zisizo sio za kuogopa,tumechoka kuchokeshwa,hatujachoka kulalama,maana hata tukanyamaza leo wengine watasema,haina haja kumfikiria mwengine ikiwa hatujajifikiria,haitawezekana kwa wengine ikiwa hatujajimilikisha,sasa ni ndiyo sasa,sasa ndiyo hasa tunahitaji kujipiga msasa,pengine bila kujari zile za jana anasa.

Ndiyo tunafanya,ndiyo hatutakiwi kufanya,hapo ikawe hatujakatazwa bali ni hatari kwa afya yako,
hiyo ni kwa kila mtu,hasa kama hapa tunapozungumza pamoja,hapa tuangalie ya zamani,hapa tukajifunze kupitia hayo,maana hata hatuwezi kujifunza bila kujua vitu hivyo yaani hayo ya mwanzo,
na ikiwa pale mwisho unaeleweka,yaani upi ni mwanzo maana tukajisahau kuwa mwishoni na kuuweka mwanzo ikiwa ni sababu,tena baadaye tukasema kila jambo,tuangalie sana hapa,tuangalie sana tunakoelekea,hata tulipotoka ikiwa ni mwanzo huko,ikiwepo mwisho kwa mmoja basi yapasa kuonyeshwa mwanzo wake.

Hatutaki kupigana na yale yasiyo na maana bora,kwani kufanya jema lililo sasa ni kutengeneza kile kilichopo baadaye,haina haja ya kujisemea na wakati walishasema,watasema na sisi inabidi tuseme maana watakao sikia na wao watahitaji kusema pia

Tunahitaji mazoezi ili kujenga miili yetu,tunahitaji maongezi ili kujenga misingi yetu,tunahitaji maamuzi ili kujenga mbele yetu,maana likiwapo hakuna linalorudiwa,sio kwa kupotea bali halikufanyika,na hapa yapasa kurudia,sasa tusijerudia kazi za nyumbani,hizi ni kazi zisizo hitaji utani

No comments:

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...