Naamka baba nishike mkono,nimeshtuka maana tusije fika
kikomo,wameshuka maana hawakulisoma somo,wamechemka kwa sababu ya kuwapo
humo,pilika na mazoea yameibua mengine,birika na vya kuzolea yamekuwa
mengine,tukaamke tukasahau iwapo kama ipo,tukatembee tukakumbuka kama yapo
yapo,yakatembea tukawepo kama ya kukumbuka yapo,pengine ni namna kubwa
sana,pengine ni asili kubwa sana,palipooza tupaache maana muda si mrefu patapasuka,embu tuone la pili hata la mwenza maana haya machache yamejichanganya
na meupe.
Kinachokuwa na msingi nikuweka nakshi,kinachokuwa na mchuzi
ni kuweka nazi,pengine tukaseme kama mwanzo ya kuijua minazi kuliko nafsi
zetu,ikawe ni kwa yaliyojaa na mengine kushindwa kutoka,hata kumwagika maana na
nafasi imekuwa ndogo hasa kwa wanaowakilisha tu,mbio zisiwepo maana hata nafasi
yenyewe ni ndogo,kile kilichokatazwa ndiyo kwanza kinaanza.
Ya jana ndiyo yaliyoleta maana ya leo,ya jana ndiyo maana
ikaja leo,muda wowote ni wa kulala hasa pale unapochoka,kwani kulala sio usiku
kama sio kupumzika,basi hapa tutaoneana,ikiwa tutapangiana hata muda wa
kulala,pengine tukafanye shuguli zetu usiku,hii ikiwa sio mabundi bali Yule aliyefanya
mchana alichoka na kwenda kulala wakati mwengine Yule akiwa amelala.
Msingi ni mkubwa kuliko kitu,kuonekana kwa juu lazima
tutafute kwa chini,tukainue hata yale yaliyopo majini,maana sasa yahitaji
kufanya hayo yote ya ndani,tumejiziba sana tuangalie tusijepumulia mipira,tumejiziba
sana tuangalie kwa wale walio na hira,kwani yaweza kufunulika na kutokuonekana
kitu hiyo ikiwa walishachukua wataalamu.
No comments:
Post a Comment