Sunday, November 18, 2012

JITHAMINI.

Haina thamani kuuzungumzia ujuzi na wakati uwezo unao, Haitawezekana kuzungumzia ya zamani na wakati mapya yapo, uwezo unaoendana na wakati ndiyo unaohitajika, moja sitajidanganya kuwa nimechelewa kufanya ya pili hoja, watakataa sasa yakuwa haijulikani lakini thamini unachokifanya pengine yakupasa kuuliza  maana unaweza ng’ang’ana kujenga barabara na hujui mwelekeo, maisha yametofautiana yanaenda na wakati wake .

Hakuna aliyeumbwa hawezi labda yule asiyejua thamani  katika maisha yake Mabadiliko yanatokana na mtu mwenyewe, wakati mwingine inakupasa kuongea peke yako ikiwa yakupasa kujua yako kabla wengine hawajayajua, maana unaweza kujulikana ndiyo kumbe si hivyo, wapo wanaoteseka kwa kufanya yaliyo sahihi na kuonekana si sahihi kwa sababu ya kutokujiamini ama vile mwingine anavyokutathmini.

Usikate tamaa katika maisha  maana kesho  inakuja kukuletea thamani yako. Ngoja,jithamini jiamini itakuwa tu. Hakuna linalowezekana bila imani usipoijua imani utahukumiwa kutokana na uelewa wako, mabadiliko siyo mafanikio au yakafanye kuthaminiwa vile utakavyo, mtu anaweza kujibadilisha kwa  lengo la kupata jambo, ukikubari kubadilika rangi kama kinyonga haitashangazwa kuitwa kinyonga ila kubadilika tu ni ishara tosha ya kuwa kuna utofauti.



No comments:

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...