Sunday, November 18, 2012

MUDA WAKO…

Hakuna anayeelewa kwani wengine wanasubiri waelewe wengine ndiyo wanafanya, bila kujali muda yapasa kufikiri pengine kuwa na wazo, Tumetofautina namna ya kupanga muda wetu,  muda haungoji mtu, ukiwa na subira utapata,pengine hata ukiwa na subira na usielewe unasubiri nini, utakuwa umechezea muda wako , unapopanda ngazi usidhani ni mlima maana kwa kupanda na kushuka, korofi nyingine hazina maana ya kuleta kuongeleka, muda wako ukifika kitaeleweka.

Leo jambo na mambo yameongeleka, kwa yale uliyoyasikia machache ndiyo ya kuweza kuukamilisha muda uliobakia, pengine ikiwa hakuna muda uliobaki basi itapaswa kuongezwa, ikiwa kuna mgonjwa  hilo ni la pili maana wa kwanza hakujiweza, ukisema upo njiani lazima ujue unapoelekea, na uliyefika ulitumia njia gani ili ikiwezekana ukawe wa tofauti. Unapofikiri fikiri na utofauti uliopo, maana kwa kujifananisha unaweza kujiona Kenge wakati wewe ni Mamba.

Ikiwa umekubari kuwa mamba ni lazima ujue kuogelea nchi kavu, mwanadamu anayeishi katika maji huyo kazaliwa huko, na akija nchi kavu lazima aogelee mavumbi. kwa Yule anayeelewa mda wake ni lazima kuufanya si ya kuhofia mavumbi, maana kama kuchafuka unaweza  usitakatishe roho wakati wa kusuuza ila ukaja muda wa kuvaa na kusema mashine hazikufua  vyema, muda ndiyo unaotufanya kuzeeka, haipaswi kuustarehesha muda wako.

No comments:

Makaya's Forum: ISHI NA YAKO

Makaya's Forum: ISHI NA YAKO : Watakwambia unabahati kwakile ulichokifanya kilichokufanya uwepo hapo,kujipa ufalme na kuzungumzia maisha...