Usipoelewa hautaweza kujua hata kama unashiriki vipi maana
kwa kutokuyapenda na kujifanya unajua zaidi kujikuta unaumia bila faida,katika vitu na watu wanaoisukuma dunia ni vile na wale wanaojifanya kujua kila
kitu,unaweza ukawa unafanya sahihi na usikute lolote limefanyika,pengine hata nguvu za
kusukumia zikawa hamna,kwa kuwa mwenye
nguvu umesahau kuangalia akiba,usipojua nini kupenda nini utafanya,wengine
huwamo ni kwa sababu ya kuvaa,pengine nguo zikichanika hakuna jipya litakalo
tokea,maisha ndiyo mapenzi na mapenzi ya mtu anayeishi yasikufanye mwanadamu
kutokuujua wakati wako.
Hakuna mtu aliyekatazwa kupenda lakini fikiri kwamba
utapenda nini au wangapi?wangapi umewapenda?je kile au yale mabadiliko
unayoyataka yametimia?penda unavyoweza ukielewa unapenda ili uishi,maisha
yaliyojawa na upendo ni maisha thabiti kama umeyaishi usijaribu kuyaacha zaidi
ya kuongeza,ikiwa kumpenda mwenzako ni zaidi ya kujipenda wewe
mwenyewe,haukatazwi kujipenda zaidi,ili mradi kwa mwenza kisiwe cha ukaidi.
Hautakiwi kuishi kwa taabu kwa sababu ya upendo,upendo
hautafutwi kama inavosemekana,upendo umezaliwa kwa kila moyo wa mmoja wetu,unapochagua kufanya
jambo fikiri kama umelipenda,fikiri endapo una uhitaji nalo ili inapowezekana
kufuta baadhi ya uchafu,maana moyo ukiwa msafi hata uje msafi ,usafi utabaki
pale pale,upendo ni asili ya mtu,jinsi ulivyo,usikimbie kimbia ya kuwa ni
lazima kupenda,ili mapenzi yakatimie,maana unaweza kuisukuma dunia ya wengi na
kuacha yako.hapa nasema umependa pasipo pendeka.
No comments:
Post a Comment