Umekuawa wakati mzuri maana kilichotakiwa
kimepatikana,katika kuona yale yasiyooonekana ikabaki muda na watu
kudanganya,maana kwa kuzunguka hapa na pale bila ya kusema,ikiwa haikutakiwa
kusemeka,hapa zitakuwa lawama,hapa tutaonana wabaya,ikiwa kitakuwapo ya
nini ishindwe kuwepo?hapa napenda kusema
kugundua hapa napenda kuhema bila kuumbua.
Unaweza kulenga mahara na kuona hapaonekani,hiyo ikiwa si ya
kwamba hakuna mwanga,ama vile ilivyo kwa wale wanga,maana imekuwa kutembea
katika namna yao wakati wa jua ikiwa ni mwanga upo hapo huleta
kutokuamua,katika kujifunza kukataa ni vyema kuanza na kuogopa,maana kama
utajifunza kukataa kuogopa basi hatimaye utapata furaha,hapo ikiwa ni kufanya
mazoezi kufurahi.si ni utofauti?
Labda kwa hili la sasa tuelewane,ikiwa limetokea sio muda wa sasa na lakini halikuweza
kushangaza,maana katika kujua imani ni lazima kujua kukataa,tena sio kwa sababu
ndiyo ni kawaida lakini kuna uwezekano wa hapana,maana napo jibu lipo,hapo
nikiwa namaana ya mtu au watu kuelewa,kama vile tulivyoelewa mwanzo,pengine
ningelikuwa peke yangu hata nisingeshinda,hapa tufikiri wote maana yanatakiwa
mazuri na mabaya ili kujifunza.
Tusifuate historia japo na nafasi kidogo na ya kwako!!
No comments:
Post a Comment