Hapa tunataka kukua,sio kutajirika bali kuwa na
furaha,pengine inapasa kujua kama tunakuwa,haitaleta maana kwa mmoja kufanya
kazi bila ya kuonekana na kukua,ingawaje tunaendelea kukua lakini tusione kwa mengine tu kukua,pengine kama
ilivyo kwa mfanyakazi anapoona kazi yake inakuwa,bila kujali ni imekuwaje,pengine
kwa muonekano kwa vile unapoondoka uzuri basi iwe katika furaha,hapa ikiwa sio
vyote vizuri vinauwezo wa kukua tena na furaha.
Katika kukua kuna
kuzoea,na endapo inafika wakati tunazoea yasiyo ya kuzoeleka hapo furaha
itapotea,ikiwa kwa mmoja kama ni mke ndiyo wa kukupa furaha,ama ilivyo kwa
biashara hapo tutakuwa,lakini katika kukuwa
haitokani na mtu zaidi ya mtu mwenywe,hata ikaonekana katika upande
mmoja kwamba wachache au mtu Fulani amekuwa lakini japo kidogo hiyo nayo
haimaanishi furaha zaidi kuwepo,zaidi tunaweza kusema katika mabadiliko ni
lazima kufanyika kila siku,na hii ikiwa ni kuleta maendeleo katika kile
chochote kinachofanyika.
Ikiwa kama ni kazi inatakiwa kukua katika mwonekano bora
basi yapasa mtu kama mtu kukua na kukuza
yale unayoyafanya,hapa inawezekana watu wakataka kukua kwa haraka,hii ikiwa
katika afya,kiakili,kimwili na mengineyo watu wayakuzayo,katika kujua kukua
lazima kuelewa ni namna gani mtu anaweza kujikuza,sio ya kwamba Fulani amekuwa
mnene basi ikaja na kueleweka kuwa amekua,kukua ni kubadilika,lakini kukua ni kuwa katika namna ile mmoja
anayoipenda,
Kwa mmoja anataka kuwa mwanamichezo na mwengine anataka kuwa
mwanamichezo lakini hii ikiwa watakuwa wanamichezo wa michezo tofauti,na hapa
ikaja maana ya kuweza kufundishana maana kwa wengine wametaka kukua lakini
haijulikani ni namna gani ambayo inaweza kukamilika ya kufanya kama ilivyo
kusudiwa,kazi yetu iwe ni kuingia na kutaka kukua zaidi katika ufanisi hasa kwa
yale tuyafanyao.
No comments:
Post a Comment