Unapofika wakati ni lazima kuacha,embu tazama wengine wakiwa tofauti na wengine,hapa tukiendelea kujua zaidi ndiyo tutagundua kwamba pengine wengine waliacha,maana haya mambo yamekuwa tofauti sana,si ya kuwa watendaji ni tofauti,si ya kuwa kuwa matukio ni tafuta,hapa tukatambua lengo kwanza.
Najaribu kushirikisha nafsi naona hazifanani,labda tushike
manati ili kuleta ushindani.hapo ndiyo ikajulikane tulipotokea,hapo ndiyo
ikajulikane ilipotakiwa maana ilipasa tuwe huko,isingekuwa na sababu bila ya
kusema nini,yaani nini ni kuhitajika pale jambo linapofanana na
mazingira.
Pengine tunahitaji mashine ili tukazifanyie kazi,ikiwa elimu ni
msingi hapo hakuna ushindani,maana kama kimeeleweka hivyo asiyekuwa na elimu
atabaki na lake,pengine ni ujuzi tu,hapa katika kusoma lazima tupate uwezo na
nadharia za kufanyia kazi na hapo ukaitwe uzoefu.
Baadaye inakuja sasa watoto hawatakiwi kusumbuka kama baba
zao ilivyokuwa,ikiwa wazee walikuwa wanatembea zaidi ya kilomita hiyo ikiwa sio
ushindani labda Fulani anahitaji kuwa namba Fulani,raha mtu anaziona za mwenzake
ikiwa taabu ipo kwake,
Pengine bila kulinganisha nafsi zaidi tutabaki na
kuendelea kuwa hivyo,imekuwa inafanana sasa kama ilivyo kwa nyoka na chura,basi
mmoja ataruka ruka na mwengine kutambaa hiyo
yote ikiwa ni safari ya maisha yao,na katika kuishi maisha ni lazima kutaka mazuri.
Ikiwa bila taabu na sababu kwanza,basi
lazima tufanye kazi,lakini hapa inategemea na taabu,maana taabu si ya kwako
tu,pengine tuchague muda wa kufurahi,na tutafurahi kweli kweli.
No comments:
Post a Comment