Monday, June 11, 2012

LENGA..

Nayawaza  madanganyifu kwa kuona yanayoongelewa,ikiwa tutaongea kwa utimilifu basi tutaongea kwa kusemelea,mengi yaliyokimbiwa yamefutwa mwanzo ikiwa ilitegemewa,pengine isiwe imekuwa bali ikakamilika kwa kuwa.

Hapa tunazungumzia matukio,ikiwa ni mara zote kwa kuanzia mwanzo mpaka mwisho tukasema ile ikawa na imekuwa kwa maana iliumbwa.

Halazimishwi paka kwa kula mchuzi wa samaki,hiyo ikiwa ni mwanzo labda kwa vile tumezoea,hapa tumezoea mengi na mengine tukadanganyika,mazoea haya yatatushindisha kwa kuwa tumetegemea hivyo,
pengine haya ni mengi sana kwa kuona,
ikiwa wametazama sana wa zamani na leo tusiseme tumeona,tunahitaji mengi sana na hili la leo liache liendelee kwanza maana imekuwa hivyo

Huu ni mtazamo kwa kuwa umeonekana,hasa kwa vijana kwa kuwa yote imekuja kwa maana,tusizungumzie leo ikiwa tunategemea kesho mbovu maaana tutafanya kuumia kwa kuwa na sehemu  iliyo na maumivu bila ya uvimbe,
huu utakuwa ni ugonjwa mwingine kabisa,hapa tukasema sijui ni nini lakini ndiyo imekuwa hivyo,ikiwa imepasa imetangulia,na wote tukiwa pembeni bila ya kuelewa maana hatujajua kama tumeweza.

Tumalize na mwisho kwa lengo la kulenga,tukapeleka pale ulipo mwisho ya kuwa tumejifunza hivyo,
yaani hayo yakiwa ni baadhi ya mazoezi,katika Fulani ikawe ni Fulani na nani,
hapa tukiwa hatuna imani,hapa tukiwa hatujasema jamani,tusipojua imeleta maana gani maana ikafika muda isije kueleweka namna ya ilivyo,hivyo inakuwa imekuwa.

No comments:

ELEWA 2

  Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye na kukataa kuelekea hata kwa ku...