Hakuna sababu ya kudanganya wakati unahitaji useme
ukweli,
uzungumze ujue kile kilicholeta maana,maana haijaja kuwa kweli bila
kudanganyana,haijaja kusema kweli bila kuchanganyana,
pengine ukaona pale umekosea kufanya vile,pengine ukaona pale tu ulipopatia,
haki iliyo ya mtu
lazima kusema ukweli,pale walipo matapeli
usogee ili kuepukana na ukweli pengine ukajua bora kwa kuchanganyana
na matapeli.
Karibu mgeni nyumbani hakujazimwa taa,karibu mwenyeji ya
ndani na njiani hakuna kukataa,pengine ulikuja mara ya kwanza na uliona bila
taa,pengine ukakataa kurudi kwa kufanya bila manufaa,kwa ukaribu jirani
angalia njiani.
Kinachoendelea ndiyo majibu hasa ya uliyoyapanga,ikiwa kama
ufahamu ni mdogo basi litagundulika hilo na sio kwamba kwamba kwa anayefeli
maisha anakufa,
hapa ndiyo unamwelewa mungu,hapa ndiyo utakaa na kujua msamaha
wa mungu maana ingawa ukashindwa yeye atasamehe,na usikatae hilo kwani umesamehewa mara ngapi?
Yatakuja mengi mengine mapya yatasemeka yalikuwepo,hiyo
ikiwa na yenyewe yamechoka huko yatokako,
yakiwa yanahitaji msaada basi
yatapenya hata kwenye nafasi iliyo ndogo yako,
ukataze yale yasiyokuwa na msingi ili uone kitakacho
bakia,
maana haitakuwa na maaana dunia kujazwa na vyoote hivi.
Sema kweli visikuchanganye na kwa uwingi uliopo usidanganye !!
No comments:
Post a Comment