Maana mengine yamekuja kama tishio,mengine yamekuja ili
yakionekana yaonekane ya kileo,wanajua wachache wale wanaoitwa walevi,maana
kila mtu anajiona yeye mwema,katika kuishi maisha yale mtu akaishi
anavyotaka,maana hata ukahamia kaburini nahisi utasikia wachache
wakinong’oneza,maana wao si hawajawahi…!!hawajui nini maana ya kuona pale,ama
kufika pale,pengine yale ni mengine yaache yaende,pengine yale ni mengine
waache watende,
Muda huo unapofika ndiyo unakuwa wakati wangu,maana pengine
ndiyo wako sasa,kama vile tunamcheka Yule anayecheza kipindi kifupi bila ya
kujua urefu ukoje,mengine ni ya lazima kuelewa pale inapotakiwa
kufanikiwa,maana kila mtu na mwenzake wanataka kufanikiwa,wakiwa na tegemezi na kwenda nayo yale waliyo nayo
na kama ni maadui basi kheri waongezeke,hapo wakiwa wawili pamoja na Yule
mshamba,maisha sio kuelewa sana sana ya kutaka kuelewa sana,maana hapo tutakuwa
tunaelewa tu,labda kukumbuka,na wala haina haja ya kuyakumbukia wacha yaendee..
Kesho tutalia zaidi ilivyo ya leo,maana hichi cha leo
tulikijua tu,pengine tumezoea sana ili kutaka kueleweka,akiyafuata Yule mjinga na mwenzake atamcheka,hapo tutapigana
na kukumbuka umoja wetu usioeleweka,kuna Yule amepata kitu na asijue nini kile
zaidi ya Yule anayepata kitu na kujua nini hiki,hiki kinatumika,zaidi ya vile
ikafikirika maana kwa mwengine anaweza kuwa hafikirii mmoja
unapofikiria,pengine sio wengi,pengine sio mengi,haya mengine tuyaache yaende
tu!!
No comments:
Post a Comment