Tuesday, June 5, 2012

TAFUTA..

Ombeni mtapewa tafuteni mtapata,imani na kweli ya mtu kumwelewa,ama imani kujielewa,vyovyote basi na majibu tukayaelewa,leo ni mara ya ngapi nairudia,imekuja sasa naurudia,kwa kuwa umekuwa ni mziki mzuri,pengine kwa kuwaona watu wakicheza,pengine kwa kuona mziki ukicheza wenyewe maana watu wanaweza kucheza vibaya kuliko mziki ulivyocheza wenyewe na hapa tukasema ni makosa ya mtegenezaji ikiwa hatukujua Yule aliyeimba,wimbo huu mtamu kweli,Tanzania Tanzania nitaaiimbimbia daima.

Kwa ufupi tukaja bila kuchoshana,kwa kirefu tukaja ili kuelewana,watu wamekuwa wakali kwa ngoma wapigiwayo,watu wamekasirika kwa ngoma na unyago,pengine tusijue kuucheza tukasema tumeweza maana wengi wao waliotangulia walikuwa wakijikweza,hizi sio stori kwa watanzania walioko jikoni,hizi sio stori kwa watanzania ambao hawaoni.

Hapo nakasirika,hapo nakumbuka,maana kweli mwisho tuweke nukta,tukija huwa tunaeleweka,tukiwapo huwa kinasomeka,kwa wale watanzania walio na hulka,sio kwa vina tukasema yamesababishika sio kwa kina tukasema tukasemeheka,pengine makosa yetu yakawa yao,pengine dhambi zetu wakabeba wao,dunia imekuwa ni chungu kwa kuelekezwa na mtandao,dunia ya kuchunguria haijafanana na sufuria zao.

Mbishi mbishie akitaka jibu mpatie,mjanja msikilize akitaka swali muelekeze,maana hawa wajanja wamekuja wengi,pengine tukawaita majina yao,lakini wasifanane na wayao,pengine tukajiita majina yetu na wala yasifanane na yao,kati na kati wametuweka pembeni yao,karibu na kati yatupasa kufikiria majibu yao,hivi ni vichache baadhi vipo kwa wao,mengine ni machache labda tuanze na kwao.

Tunaondoa uwoga kwa kuomba kilichopo,cha baadaye wacha kije kwa msimamo uliopo.sikubali leo kiduku kukitilia mkong’oto,sikubali leo kwa watanzania kuishi katika maporomoko,tukumbuke leo kwangu kesho kwako,tukumbuke ya leo yangu kesho yako.

tafuta,tafuta iliyo ya kwako..Tafute kile kilicho chako!!

No comments:

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...