Monday, July 30, 2012

MVUTO.


Navutiwa na kuona watu wanafuraha maana ni furaha kwangu pia,inanivutia kuona watanzania wameamka na kuacha kulalama,inavutia kweli kwa kuona yale magumu angalau watu wameanza kuyafanya,hapo hata kama hayawezekani lakini kuna imani na tumai ya kuliweza japo moja,hii ni kwakuwa tumeweza kukua katika upande fulani wa maendeleo,ikiwa pamoja na vizazi kuongezeka.

Pengine inavutia sana kwa kuona watu wakijishugulisha kwa vile maisha ni magumu,maana ingalikuwa ni kula tu isingelikuwa na maana ya kuvutiwa na majengo na mambo ya mjini,ingawaje tunasema mjini kuna upatikanaji wa mahitaji kiujumla na zaidi ni haki tumevutiwa na vitu hivyo,pengine tunataka tuwe nani lazima tufanye vile vinavyotuvutia,labda ikija badaye vitarudisha fadhila ikiwa na sisi tutavutia.

Unapofanya yale ya kwako ni kufanya ngazi nyingine katika kupanda maisha yako,tunaposema maisha ni yako ya maana ukifa leo wengine watabaki ikiwa walivutiwa tofauti,ingawa ni vigumu sana kwa mwanadamu kusema kile kinachomvutia kabla ya kufanya,pengine wengine wataogopa,wakisema mbona ya kwako hukusema,haihitaji nguvu katika kuonyesha kile mtu unachopendezwa nacho ni akili na msimamo ya kuwa ni wazi kufanyika.

No comments:

ELEWA 2

  Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye na kukataa kuelekea hata kwa ku...