Monday, July 23, 2012

KAMPUNI.


Maana wao wananunulika tu,hiyo ikiwa ni kama bidhaa,tena kwa noti mbili zenye thamani moja,hii kweli ni kioja..tufanye noti moja ikawa mfano wa kununulia bidhaa moja na tena ikaja noti nyingine na namna ile ilivyo na biashara kufanyika hapo tunasema kuna uharamu,tena uharamu mkubwa sana bila kugundua maana nitapenda kuelewa wageni wanapokuja kuingia kwenye kampuni mnatoa zipi,zile za kwanza ama hizi zilizofuata,maana pengine zikija za tatu tusiwe na mashaka na za pili,maana za kwanza si zilikuwepo.

Leo ndugu zangu makampuni yanaongezeka,watu wanauza watu na sio mali,maana kama hautataka kufanya kazi katika kiwango cha chini basi kafe njaa,wewe bisha kesho ikutokee maana usiiombee..kesho watoto wetu watakuja na hasira sana maana hata tukishindwa kuwa na kampuni,nchi imegeuka kuwa kampuni,ya nini nishindwe kuwa na nchi yangu,pengine ni wewe,pengine ni mimi  endapo tunakubali ,nina mengi sana kuhusiana na hapa na kama kuna mahala zilibaki basi na sisi tugawieni,maana mbona zipo nusu nusu..au mnasemaje wateja? 

Hapa ni mengi tu jamani mmeyamezea,sijui ni baba zenu wamewaambiaa?maana bora hapa vile viboko vya mchungwa,pale mchungaji anapokuwa hajui kuchunga..haya yamekuwa mateke ya kuambiwa’aya pangeni mstari..kila mmoja anakuja hapa anapigwa teke la tumbo moja moja anaenda zake kulala'..hapa kila mtu angebaki nyumbani kwake ‘kura’ ampigie nani?ndugu zangu muda huu wanosikia wachache sana,ila itakuja kueleweka,maana  hayo yatakuwa ya ‘kodi’ itabidi tuyamalizie ndani ya kampuni..

No comments:

ELEWA 2

  Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye na kukataa kuelekea hata kwa ku...