Kweli ikifahamika kweli itaumiza,maana wakubwa wamekuwa
kama watoto,na watoto wanashindwa kuelewa maana wakubwa wamedanganywa na vile
walivyotakiwa kudanganyia watoto ni mchanganyiko maisha
magumu mtu anajiuza nafsi kwa kidogo kitu ni chakula ndiyo tena ukibisha sana utanunua hata kavu.siku
hizi si kwa wanawake tu ndiyo maana hata ikaruhusiwa ndoa za jinsia flani,maana
hata hawa hawa wanaume wananunuliwa na hii sielewi sijui ikiwa kununua na kuuza
ni tofauti?maana Yule anayenunua danganya toto ili akadanganye toto naye
kadanganywa na muuzaji,hapo baada ya kugundua mtoto amedanganganywa kweli..
Leo tunataka barabara ili tuendeshe magari yetu pale
sebureni,watoto wakijinadi kwa wazazi si kuna yale magali ya ramani?samahani
watoto wenzangu wa uswahili haya yanafuata yalipoelekezwa,pengine yalikuwa
machafu basi yanaenda mtoni kuoshwa,na ikiwezekana huyo muoshaji anayehitaji
atapata na mengine bure,ila lazima atie saini,sasa umepewa au mumebadilishana?maana
watu wanakaa vyuo miaka saba mnataka muwashibishe na makaratasi..?hakuna mtu
anayependa kula cha mwenzake,ndiyo maana kila mtu ana kwake,vile vya kwake kula
na watoto wake,ili wasidanganyike..
Nani huyo asiyedanganyika maana wanaodanganya wanajua,kwani
ile huwa ni tabia,pengine atakaa pembeni na kujifikiria baada ya kujua
ukweli,pengine inauma sana ukifikiria ulipodanganywa kitoto toto,achana na hilo
imakuwaje taifa zima kudanganyika?maana hapa bila kujua matokeo ya kile
tunachokishangilia,tutakufa sisi na kubaki wao,tunaweza kukubali kudanganyika
kwa kusema ni ‘Shida’bila ya kujua hata kama ulizaliwa kwa shida,kama kuna mtu
alizaliwa kwa raha basi huyo ndiyo anawapa shida wengine..
No comments:
Post a Comment