Wednesday, September 26, 2012

UKAMILIFU..


Kuna ulazima wa kuchagua wewe ni nani ikiwa unataka kukamilika,pengine ukiwa na malengo,mipango yako iliyokamilika na ikitakikana kufanyika ama imeshafanyika na wanadamu kuona namna ya vile ilivyotendeka ikiwa wao ndiyo huleta makamilifu ya sifa,chako ni chako,kichafu na kisafi ni vyote vilivyo kamilika ikiwa ni katika namna inayotakiwa,kwani pale anapopenda mmoja mwengine anaweza penda hapo ilipo ya kuwa ni katika kukamilisha matokeo.

Mabaya huwa ni mazuri kwa kuwa yameweza kuwa na uwezo wa kuwa mabaya .kukamilika ni namna ya kitu kilivyo,na endapo hakijakamilika ni lazima kupeana namna ili inapokuwa inataka kukamilika iweze kukamilika katika namna na maana ya vile ilivyo.pengine ni utofauti unaofanya mtu asiwe na ukamilifu,akiamini yeye ndiyo yeye,kwa kuweza jambo na wengine kushindwa.hayajawa mashindano maana hata muda wa mchezo wenyewe unapangwa na  wewe mwenyewe.

Maisha yanajengengeka na namna ya ukamilifu wako,ikiwa haujatimiza jambo na unahisi ya kwamba si mkamilifu basi jaribu kukamilika kwa kuweka kile unachokihitaji kukifanya kuwa kama ni baba au mama maana hakuna pengine pa kuwapata,si ndiyo ikawe fulani ni mtoto wa fulani na fulani,si vile ikawa haieleweki  kwa kutokukamilisha uzazi,na ki ubainadamu wengi hupenda kujikamilisha na kutokukamilisha ya wengine.wakijua yao yamekamilika.

No comments:

ELEWA 2

  Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye na kukataa kuelekea hata kwa ku...