Friday, February 17, 2012

Makaya's Forum: USHINDI…UNAHITAJI KUJIANDAA.

Makaya's Forum: USHINDI…UNAHITAJI KUJIANDAA.: Maandalizi ni malengo katika kutekeleza yale yanayotaka kufanyika,ikiwa katika mmoja mmoja hadi pale ikafikia kundi,hii yote hutokana ikiw...

USHINDI UNAHITAJI KUJIANDAA.

Maandalizi ni malengo katika kutekeleza yale yanayotaka kufanyika,ikiwa katika mmoja mmoja hadi pale ikafikia kundi,hii yote hutokana ikiwa kila mmoja aliyepo naye akiwa na timamu ya kutaka kufanya jambo lisiloonekana na likaonekana kama ni jambo limefanyika,ikiwa tu,kwake naye lilikuwa ni lengo.katika kujiandaa kuna mengi ili kufikia mwisho,mwisho ndio timilisho la maandalizi ikiwa hapo ndio tunaweza kujua kama ni maandalizi yalikuwa mazuri au la kuwa vyote hivyo inategemea na mtu kufuatana na (ma)lengo lake,USHINDI ni pale mtu anapotimiza lengo,ikiwa tu alijiandaa,hata mara nyingine ushindi huja kwa watu wasio jiandaa,na hiyo siyo ya kuitegemea ikiwa ni bahati,wala hatuwezi kusema ushindi usio kuwa wa kutegemea ni ule wa kukosa.tuna hitaji ushindi ili kutekeleza mambo yetu,tunahitaji kujiandaa ili tuweze kushinda.

useme ni wangapi wanaojiandaa,na utakuta ni wote maana kila mtu ajiandaaye hujiandaa mwenyewe,yule anayeandaliwa ni lazima ajue kuandaa pia kwani endapo akishinda hataweza kuulinda ushindi ya kuwa hana maandalizi useme wale wanaoamka ndio wa kuweza kujiandaa kwani walikuwa wamelala,na wale walio lala ni kuwaamsha ili waweze kujiandaa ikiwa ushindi mtu anaupata pale hasa alipojiandaa mwenyewe,maana unaweza kuja kidogo ama ukazidi na kufanya karaha,kivingine ikawe ni ile bahati maana haukuwa wa maandalizi yale,ushindi wa bila kuongea unaweza usisikike,na mara nyingine ukiongea sana wanaweza kunyamazisha,maana wao hawamjui mungu na labda nisiseme hivyo zaidi iwe wanamjua mungu wao.pale unapokosa ndio pale majibu yalipo,ni kama pale unapopata ingawa haitaweza kulingana,ni tofauti ya kuwa moja ni ushindi nyingine ni kinyume yake.

Kile kinachoweza kuzuilika ni kile kisichopangika,maana kitakaaje?kama maji hupita kokote,hata yakaleta uharibu hata ikawe sio lengo kubomoa,pale yanapobomoa yenyewe ushinda ikiwa yalipotoka yalikuja na yakabomoa,labda yangeenda pengine ili ungejua kuwa haikuwa lengo,na iweje yangefanikiwa ungeeiita ni bahati yake,kwa yule anayejenga ukuta kwa ajili ya kuzuia maji hayo anajiandaa,kwa yule anayeyasubili yaingie mpaka ndani basi atafanikiwa,maana amesubiri hivyo,muda mwingine huwa inakuwa haiwezekani,ikiwa katika hali ya kawaida hasa mtanzania ikiwa wengi hatufahamu mazingira yetu,ikiwa ni miili pekee tunayoifahamu,tukisahau mazingira mengine tukataka afya bora,hii itakuja kwa kunenepa ikiwa ni bora basi itakuwa bahati,siwezi kusema sana hapa labda tungeulizana nani au na flani wanapenda nini,maana utofauti upo,na matokeo sio maandalizi,ikiwa yenyewe yakawe na kusudio la kuleta ushindi.

Vizuizi ni haki kuviweka pale unapojiandaa.lakini ni pale tu utakapo jua ni unazuia nini,Katika utofauti wa malengo tuseme yawe yanayofaa yote,yakitofautiana kwa mabaya na mazuri kwani tunaweza kuchanganyana kwa muda mbadala,endapo yale yasiyokuwa ni malengo kufanyika kama malengo wakati Fulani,yule anayejiandaa ndiye anayejua lengo hasa,labda na ije tofauti..hapo tunasema anapanga mungu.
mda mwingine lawama hazifai labda ujue nini unachokifanya,maana kama ni unajiandaa na imetoka kipindi maandalizi yakawa magumu unaweza kuyakimbia endapo haujafahamu unajiandaa na nini, 

'tutaishia kunawa maji ikiwa na chakula tumekiona mbele yetu'.
kwani hata meza zenyewe waligeuza kitambo!!

By:          Benson G, Makaya,
Tel:         +255 714 33 66 57.
email.   bensonsmakaya@gmail.com

Thursday, February 16, 2012

Makaya's Forum: BINADAMU ANAPOTEMBEA..!!

Makaya's Forum: BINADAMU ANAPOTEMBEA..!!: Binadamu anapotembea anaangalia wapi..?maswali mengine bwanaa!!tuseme ni kushoto ama kulia,wale wenye uwezo huangalia kote,hatuwezi kuan...

BINADAMU ANAPOTEMBEA..!!



Binadamu anapotembea anaangalia wapi..?maswali mengine bwanaa!!tuseme ni kushoto ama kulia,wale wenye uwezo huangalia kote,hatuwezi kuangalia kote bila kuwa makini,yaani utambuzi kiujumla kujielewa.
Hatuwezi kusema wote tunaangalia kote,kwani wote sio wale tunaotembea,na hii haiwezekani,ni kweli tunatembea,na ni kweli sio wote.muda wote tuseme sio haki kutendeka lakini ndio inatendeka,hakuna yule atendaye lisilotendeka na likaitwa tendo bora,matendo ni yale hasa tuyatendayo,ndiyo na yote sio mageni,sio yale ya kushoto wala kulia,ya chini yatabaki huko maana hayana haja ya kuyafikia,wengine watasema hawajawahi na kama kutenda ni kuwahi basi wote tumechelewa.

Sio yale tuliyonayo tukimaanisha tumeyatenda,hata kama tumeyatenda si yale tunayoyasema tumeyaweza,yapo yote na tuliyoyashindwa,tunapotembea sio miguu tu kwani hata akili nayo hufanya kazi kubwa mikono nayo pia ikatembee,muda mwingine tutembeze na mioyo yetu.Wengi watu hatuelewani,tumesahau kuwa hata wale wa zamani waliandika,ndiyo wale waliotembea wamefika hadi hapa,waliacha akili zao zinatembea,sasa wengine wakiangalia wanavyotembea wanapofika ni pale walipo,mahala na muda wanautaja kama ulivyo,ya kuwa wapo hapo.Kama matembezi ya maelfu yameshindikana basi hatutaweza yoyote,wataweza wachache,ni kama ilivyo shule kwani chochote kile sio cha kusoma,cha kusoma huwa wanaambiwa soma hapa,elewa pale unaposoma,jua unachokisoma sio kile unachokiona,macho hayadanganyi lakini kwa dunia jinsi inavyotembea haiangalii mwanadamu amesimama ki namna gani.

Tusherehekee vyote na tujipongeze hasa pale tunapoona tumeweza kukimbia,ikiwa ni wengi wanapenda kuwahi,labda tutembee haraka tu tusikimbie,yakuwa hatujui tunakimbilia wapi,tusije kimbilia bomu,bomu hufyatuka endapo pale kunakuwa hakuna uangalizi na yule anayekimbia uangalizi wa sehemu aliyopo ni mdogo sana,tukubari yote ya kuwa tunauwezo wa kukataa yote,kwani hata tukisema ni kutaka ufikiriavyo wewe lazima wengine watakubari huku wengine watakataa,labda tuseme haina haja ya vyote hivyo,watakao kataa na kukubari vyote kheri kwani yule anayekataa njia hii anayo nyingine,yakuwa anataka kupanua uelewa,ili asaidikike atakua ametembea.

TEMBEA UYAONE..

By: Benson G. Makaya,
Tel:  +255714336657.
Email:bensonsmakaya@gmail.com

Wednesday, February 15, 2012

Makaya's Forum: SAUTI KALI...

Makaya's Forum: SAUTI KALI...: Sauti zimezidi kuwa kubwa,zimejaa na chumba ni kidogo,ikabaki ikawa na sasa imekuwa ni mtafaruku,sio mda wake huu,ingawaje kihalisi imet...

SAUTI KALI...



Sauti zimezidi kuwa kubwa,zimejaa na chumba ni kidogo,ikabaki ikawa na sasa imekuwa ni mtafaruku,sio mda wake huu,ingawaje kihalisi imetimia,labda upate mawaidha,yaani utiwe moyo,unaweza kuleta usikivu na ikiwa hivyo ukakaa chini na kufikiria,lakini isiwe hadi kufika kilele,maana hapo nguvu zinapungua,uwezo wa kufikiri unatokana na nguvu pia,na hapa ikaeleweke sio wazee wanawasemea,ni vijana mkaweze kukaa na kuweza tazamia,milango usifunge,makelele yatakuzidia,ingawa ulikuwa hujui ya mwanzo yaliyokufikia,usingeliyafahamu hata kwa nguvu kupayukia,vile sauti  kuwafikia,labda ufikirie  na kwa makini kusikilizia,tunavutiana kwa namna isiyowezekana,na hii itatupelekea kukaa kimya sana,hata ukaweka utamu wa lugha kwa jinsi zinavyojulikana,haita leta msingi zaidi ya watu kupigana,ikiwa wengi wanasoma shule yale ya mtaani yamekuwa hayana maana,ingawa ni yetu ya leo na wala siyo ya jana,tumekuwa wazembe wenyewe haina haja wa zamani kuwatukana,hata ukatembea mbali kutafuta nyama,majani yatakuotea karibu na kuchafua bila hiyana,unahangaika kwa pesa na zimekuwa hazina dhamana.ikawekwe barabara iliyo jaa rami kama mkeka,faida ya nani kama siyo ya malaika?maana imekuwa ikipita siku chache na kubomoka,sijui ni raslimali au ujuzi wa kutokujali,ntaongelea machache yasiyo kuwa na hali,siyo yale ya wanaume wasio lijali,ni wazi kwa mwenye vichache apaswe kuongezewa,maana ni anavyo vichache kweli,ile ya mwenye nacho kuongezewa ni ya watu hai,wafu lao kaburi,na maombezi ndiyo nyongeza yao,nao wafike salama mahala pema mbinguni.

Mambo yanapozidi kuwa magumu ndiyo mwanzo hasa wa yale maraisi,ni kile alichonacho mwanaadamu,ingelikuwa kila mtu anazaliwa anaambiwa nenda kaendeshe baiskeli sidhani kama angetoka mtu na kusema ni rahisi,tena bila kufundishwa..kwani hata hiyo baiskeli yenyewe ingelikuwa ngumu kuitaja bila ya kuiendesha,mbadala wa matembezi yanayotoa sugu miguuni ni mapumziko ya viungo hivyo,hawakuchoka hawa wanaotengeneza baiskeli tangia mwanzo,wakarahisisha mpaka wakaweza kusafiri nazo,sio uwezo ni namna ya kuweza na kigezo,inapochakaa baiskeli makelele huanza,ukapita mikoa mbalimbali kama mbeya na mwanza,baiskeli zinapokuwa kitu cha kwanza,ni maendeleo haya kwani hakuna aliyeyakataza,barabara zikaonekane hazina maana kwani hata mijini ukawawekea bado ni mtafaruku kwa wao kupita yapitapo magari,na ikiwa ni mmoja wapo watakupigia kelele ya kuwa unaleta foleni.mambo ya mjini ni mengi,lakini mji huo huo ndiyo kijiji,sasa uchague moja kati ya kijiji au mji,maana unaona watu wanatoka morogoro wanakuja kutibiwa hospitali ya mkoa dare s salaam,wale wa dar na wenyewe wanafanya hivyo,mshangao kwa wale wanaosafiria nje magonjwa yao,kenda rudi ni maralia na baada ya hapo ni mapumziko..kule hakuna kelele tatizo hapa ni pale unapopumzikia kodi za watu huku wenyewe wakiwa hawazijui hata haki za kwenda hospitali,sauti kali huleta ugomvi kwa kutokuelewana,na baadaye ni vita.

Macho yasitoboke,masikio yameziba sasa wanaopiga kelele waendelee,maana hata ukikataa sauti zenu hazipayuki na haipiti siku,pigeni kelele wanafunzi na mwalimu akija mwambieni ni kwa sababu hakuwepo,maana hujifanya kuelewa yao mara nyingine,hata hivyo ikiwa ni namna ya kutaka kujua ni nini kifanyike mda huo.

By:Benson G.Makaya
Tel:+255714336657
Email:bensonsmakaya@gmail.com


Tuesday, February 14, 2012

Makaya's Forum: MAKUBWA ZAIDI YA FIKRA.

Makaya's Forum: MAKUBWA ZAIDI YA FIKRA.: Makubwa ni neno linalosifia kitu,kitu yaweza kuwa ni kitendo,kifaa,mawazo,nafsi ya mwanadamu mwenyewe na mengineyo mengi yanayomzun...

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...