Unapotafuta na kuhitaji kitu wakati Fulani pale mwanaadamu anapoihusisha nafsi yake kupitia mapendo ,nikisema watu wanaenda tu kutafuta maisha maswali yanaweza kuwa ni mengi tena isiwe ni kwenda tu baada ya kuulizwa unatafuta nini hata sielewi kama yalifichwa ila itakuwa ni ile sehemu iliyopo katika akili zako za kuweza kutafuta kitu kilichopo,kama ilivyo hesabu unaweza ukawa unajua majibu na usijue nini njia yenyewe,kila jibu linatokana na yale yaliyopo njiani pia ikiwa mtu ameishia gerezani kwa ajili ya kuiba si kwamba naye aliiba katika njia zake zote,yaweza kuwa alienda kwa sababu aliiba katika njia moja na watu wakapata kujua kuwa Yule ni mwizi,ni vigumu kuishi ukiwa unajua hupendwi,hata ikawa unapendwa basi chuki zikawa ndani ya watu wengine juu yako,hauwezi kujua wanaokuchukia bila ya wewe kuwa na chuki pia,ni kweli kwani hata ukamwona simba anapita barabarani kitakacho fuata ni kukimbia,na kama itakuwa wataamua wachache ndiyo wakaweze mdhibiti simba huyo,au useme vyovyote itatokea kwani matokeo huwa ni tofauti daima kama ilivyo kwa wanaotoa majibu na sio majibu yenyewe.katika maisha hakuna kujaribu zaidi ya majaribu
maisha yenyewe hayatafuti,yapo yamekaa yakiwa yana mengi mengine yapo mbali,yameonekana kwa walio lakini kwa wachache hawana budi kuinama uvunguni,kwani limeshakuwa sharti kwa kile cha uvunguni unachokihitaji kukiinamia,miguu haiji mikono bora endapo mikono ipo,na kama ungelizoea kula majani au miti nadhani juhudi za kupanda miti zingeongezeka,unatafuta pesa na hauelewi ununue nini,ikiwa unataka ununue.unatafuta pesa unakuwa na malengo ya kufanya vitu na vitu hivyo vinakuwa kama havikupangwa,kumbe pesa sio kitu pekee kinachomuzesha mtu kufanya jambo,ikiwa unaweza kuwa na nia ya kutaka kufika mahala katiks maisha,unaweza kujua ni nini unahitaji na tatizo sio kutafuta,sio nguvu,wala mtafutaji,ikiwa mtafutwa yupo na hata hizo sababu za kutafutia zinaweza zisiwe na maana zaidi endapo mtafutaji hajui pa kutafutia.
Ndugu yangu kwa chochote kinachotafutwa ni lazima kiwe na mlengo wa mafanikio,ndiyo hata watu walio na utajiri wamefanikiwa katika upande mmoja ya kuwa nao wana uwezo wa kupata kile wanachokitafuta,kumbe pesa ni daraja la mafanikio,na mafanikio ni mafaniko yenyewe.shabaha na mlengo unahitajika tena ikiwa mimi au wewe ndiyo unahitaji mafanikio,sijui itakuwaje ukipata unavyovitafuta,sijui unatafuta nini maana kwa kujua unachokitafuta utaweza kuelewa itakuwa ni namna gani pale utakapo pata,na ukipata ijulikane,maana kama ni pesa wengi wamezipata na wanazo ikiwa haujasikia mmoja wapo akisema nimezipata.lakini ya kuwa mtihani wanafanya wengine,wanasahihisha wengine na washangiliaji watakuwa wengine pia,kwa yule anayefanya mtihani ijulikane amelenga kupata maksi gani.
By: Benson G, Makaya,
No comments:
Post a Comment